DC Tandahimba ahimiza usajili wa wakazi

MTWARA: MKUU wa Wilaya ya Tandahimba, Michael Mntenjele amewaomba madiwani pamoja na viongozi wengine wilayani humo kuendelea kuwakumbusha wananchi na wageni umuhimu wa kujiandikisha kwenye daftari la wakazi ili kurahisisha ufuatiliaji pindi linapotokea tukio.

Hayo yamejiri katika kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba kuhusu kupokea taarifa za kata kwa robo ya pili ya mwaka wa fedha 2025/2026 kilichofanyika kwenye halmashauri hiyo.

Amesema serikali imetoa agizo kwa wakazi wa kila kijiji, kitongoji na mtaa kujiandikisha kwenye daftari la wakazi huku wageni wakitakiwa kujisajili ili kufahamika sababu ya kuingia katika maeneo husika pia kutambua wageni wanaoingia katika maeneo hayo kwani endapo tatizo litatokea itakuwa rahisi kuwafuatilia.

“Wakati mwingine wageni hatuwatambui na hatuwafahamu mbaya zaidi tunapokea wageni kwa sababu amejitambulisha na kujionyesha kuwa mwema hata kukupa pesa unampokea tu bila kutoa taarifa, bila kujua, hili ni jambo hatari sana,”amesema Mntenjele.

Katika hatua nyingine, ndani ya baraza hilo baadhi ya madiwani waliibua hoja ya upungufu wa watumishi pamoja na baadhi yao kuhama vituo vyao vya kazi hali inayosababisha halmashauri kuwa na uhaba wa watumishi katika baadhi ya kata.

Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Aziz Suleiman alisema changamoto ya watumishi kuhama tayari wameifikisha kwa mkuu wa mkoa wa Mtwara ambapo alisema mkoa unaendelea kushughulikia changamoto hiyo, huku sababu kubwa ikitajwa kuwa ni baadhi ya watumishi kutokupata stahiki zao kwa wakati.

Habari Zifananazo

3 Comments

  1. I just came across this amazing way to earn $6,000-$8,000 a week online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
    .
    Follow Here ……………………… https://Www.Cash54.Com

  2. I am making a real GOOD MONEY (300$ to 400$ / hr )online from my laptop. Last month I GOT check of nearly 18,000$, this online work is simple and straightforward, don’t have to go OFFICE, Its home online job. At that point this work opportunity is for you.if you interested.simply give it a shot on the accompanying site….Simply go to the BELOW SITE and start your work…
    .
    This is what I do………………………………….. ­­­https://Www.Payathome9.Com

  3. I am making a real GOOD MONEY (300$ to 400$ / hr )online from my laptop. Last month I GOT check of nearly 18,000$, this online work is simple and straightforward, don’t have to go OFFICE, Its home online job. At that point this work opportunity is for you.if you interested.simply give it a shot on the accompanying site….Simply go to the BELOW SITE and start your work…

    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→ https://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button