Watoto 70,000 huzaliwa kila mwaka Temeke

DAR ES SALAAM: HALMASHAURI ya Wilaya ya Temeke iliyopo jijini Dar es Salaam inakabiliwa na changamoto ya ongezeko kubwa la watoto kutokana na kasi ya wajawazito kujifungua ambapo kwa mwaka zaidi ya watoto 70,000 wanazaliwa hali inayoathiri katika sekta ya elimu na afya

Akiwahutubia Madiwani wa Kata ya Temeke Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sixtus Mapunda amesema kutokana na kasi hiyo wamelazimika kuja na mipango ya haraka ikiwemo ujenzi wa hospitali mbili za rufaa na kufannya Temeke kuwa na hospitali 5 za rufaa.

Pia ujenzi wa shule za maghorofa ili kuendana na kasi ya kujifungua ya kina kama ambao kwa siku watoto zaidi ya 100 wanazaliwa .

Aidha, Mapunda amewaagiza Madiwani wa kata za Temeke kuanza kutoa elimu na kusimamia utekelezaji wa maagizo ya Rais ya kuondoa wafanyabiashara wadogo katika maeneo yasiyo rasmi ikiwemo barabarani katika maeneo ya Mbagala na Tandika.

Wakizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani Mstahiki Meya wa Manispaa ya Temeke Uzairu Abdul Athumani pamoja na Mkurugenzi wa Temeke wamekiri mbele ya baraza hilo kupokea maagizo ya serikali huku wakiahidi kufanyia kazi maagizo hayo ambayo ni pamoja na kuanza kwa utekelezaji wa kubuni vyanzo vipya vya mapato ili waweze kutekeleza miradi ikowemo ya kujenga upya eneo la Tandika na Kurasini.

Katika hatua nyengine Mkuu huyo wa Wilaya ya Temeke ameeleza kuwa mipamgo ya Temeke ni kuachana na barabra za changarawe na kuhamia katika ujenzi wa barabara za kiwango cha lami kwa mitaa yote ya Temeke ,ujenzi wa nyumba za maghorofo pamoja na kujenga jengo jipya la mkuu wa wilaya wa temeke ili kulisha wawekezaji katika eneo la sasa.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button