Taasisi yavutiwa uwekezaji ujenzi vyuo vya VETA

KAGERA: Taasisi inayohusika na Elimu ya Juu Afrika Mashari (IUCEA)imevutiwa na uwekezaji unaofanywa na serikali juu ya ujenzi wa Vyuo vya Ufundi Stadi (VETA)  na kudai kuwa program zinazoendeshwa na vyuo hivyo zinatoa fursa za ajira kwa vijana katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Viongozi mbalimbali Kutoka vyuo vikuu Afrika Mashariki wanaounda umoja huo wametembelea chuo cha VETA Mkoa wa Kagera na kujionea program mbalimbali za ufanisi ambazo zinatoa fursa kwa vijana kujajiri.

Profesa Maw Michael, Katibu Umoja wa IUCEA alisema kuwa kwa miaka ya nyuma umoja huo ulikuwa ukjihusisha na vyuo vikuu lakini miaka 8 iliyopita umoja huo ulianza kujihisisha na vyuo VETA kwa lengo la kuhamasisha vijana wa Afrika Mashariki kubadilishana uzoefu katika fani mbalimbali na kujaribu kuweka sera za kielimu zinazofanana ili kurahisisha ajira katika mipaka yote ya ukanda huo.

Mkurugenzi wa Mafunzo wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Tanzania, Dk Abdallah Ngodu, alisema Serikali ina lengo la kuhakikisha vijana wasiopungua 120,000 wanahitimu mafunzo ya ufundi stadi kila mwaka ili kuimarisha nguvu kazi ya taifa.

Alisema kuwa katika mwaka uliopita

jumla ya vijana 86,000 walihitimu kutoka vyuo mbalimbali vya VETA nchini, hatua inayodhihirisha ukuaji mkubwa wa sekta ya elimu ya ufundi stadi ambapo alidai kuwa hadi sasa nchini kuna takribani vyuo 80 vya VETA vinavyotoa mafunzo, huku vyuo vingine 65 vikiwa katika hatua mbalimbali za ujenzi.

Alisema lengo la ziara ya washirika hao ni kujionea uwekezaji mkubwa uliofanywa na Tanzania katika sekta ya ufundi stadi pamoja na kubadilishana uzoefu wa namna bora ya kukuza ujuzi kwa vijana wa Afrika Mashariki.

“Serikali ina dhamira ya kuhakikisha elimu ya ufundi stadi inawafikia wananchi wote bila ubaguzi, VETA inatoa nafasi kwa jinsia zote pamoja na makundi maalumu ili kila Mtanzania aweze kushiriki katika ujenzi wa uchumi wa nchi,” alisema Ngodu.

Kwa upande wake, Mratibu wa Kanda ya Afrika, Dk Cosma Chawana Joseph, alisema kuwa kwa sasa nchi nyingi za Afrika zimeongeza uwekezaji katika sekta ya ufundi stadi kwa kuwa ndiyo njia kuu ya kujenga ujuzi, maarifa mapya na nguvu kazi ya vijana.

 

Alisema ziara yao katika Chuo cha VETA Kagera imewapa fursa ya kujionea kwa vitendo namna Tanzania ilivyowekeza kwa kiwango kikubwa katika vyuo vya ufundi stadi, hasa vyuo vikubwa vya VETA.

“Nchi za Afrika zinaendelea kushirikiana katika kuboresha elimu ya ufundi stadi. Hakuna ushindani, bali tunalenga kudumisha ushirikiano imara kwa ajili ya maendeleo ya pamoja ya bara letu,” alisema Dk  Chawana.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button