Vijana wanufaika mageuzi ya mikopo

SERIKALI imetangaza kupunguza masharti ya upatikanaji wa mikopo ya Mfuko wa Maendeleo ya Vijana, ikiwemo kuondoa sharti la lazima la kuunda kikundi ili kijana aweze kukopa.

Akizungumza Machi 2, 2026 mkoani Mtwara wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Vijana, Waziri wa Ofisi ya Rais, Maendeleo ya Vijana, Joel Nanauka amesema hatua hiyo inalenga kuhakikisha kila kijana ananufaika na mikopo hiyo bila vikwazo.

Katika tukio hilo, vijana wamekabidhiwa bajaji, pikipiki na maguta vyenye thamani ya shilingi milioni 140 kupitia CRDB Foundation kama sehemu ya mkakati wa kuwawezesha kiuchumi. SOMA: Bodaboda, bajaji watakiwa kuanzisha vikundi kujikwamua

Aidha, Dk. Nanauka amesema Serikali imetoa muda wa miezi mitatu hadi sita kabla ya mkopaji kuanza kurejesha mkopo, hatua inayolenga kurahisisha marejesho na kuzuia vijana kukimbilia mikopo yenye riba kubwa.

Naye Meneja Mwandamizi wa CRDB Foundation, Baraka Kihalo amesema wanufaika wa mpango huo ni vijana 40 waliopatiwa pikipiki 15, bajaji 5 na maguta 5, huku gharama hizo zikijumuisha bima pamoja na usajili wa vyombo hivyo.

 

Habari Zifananazo

2 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button