Bodaboda, bajaji watakiwa kuanzisha vikundi kujikwamua

DAR ES SALAAM: MKUU wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo amesema serikali itaendelea kuwaunga mkono maafisa usafirishaji (Bodaboda na Bajaji) katika Mkoa wa Dar es salaam kwa kusajili vikundi ili waweze kujikwamua kiuchumi na kuacha kukaa vijiweni hali itakayosababisha kuanza kutumika vibaya.

Mpogolo ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa saccos ya maafisa usafirishaji hao wa bajaji na bodaboda (MAUPIDA)uzinduzi ambao umekwenda sambamba na elimu ya mikopo.

Mpogolo ameeleza kuwa serikali ya awamu ya sita imejizatiti kuhakikisha vikundi vyote vilivyosajiliwa vinapata mkopo na atahakikisha anafuatilia kuona kila mmoja ananufaika mkopo kwa kuongeza mtaji na kujiinua kiuchumi.

Amebainisha kuzinduliwa kwa Saccos hiyo kutasaidia kufahamika vizuri serikalini na taasisi za kibank kwa kuwa tayari watakua katika mifumo mizuri ya kisheria na taratibu.

Aidha, Mpogolo ametumia nafasi hiyo kuwataka vijana kujiunga katika vikundi ili kujikwamua kiuchumi na kuacha kukua vijiweni hali itayopelekea kuanza kutumika vibaya.

Pia amewahakikishia maafisa hao usafirishaji, ombi lao juu ya vituo vya kufanyia huduma ya usafiri kwa mjini linaendelea kufanyiwa kazi ili waweze kufanya kazi zao vizuri.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button