TMRC kuwawesha wananchi kupata makazi

SERIKALI imesema itaendelea kushirikiana na taasisi za fedha kuiwezesha sekta ya fedha kupata mikopo yenye gharama nafuu ili kuisaidia jamii ya kipato cha chini kumiliki makazi bora. Naibu Waziri wa Fedha, Mshamu Ali Munde alisema hayo hayo Dar es Salaam akizindua huduma ya mikopo midogo ya makazi Dar es Salaam kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Khamis Mussa Omar.
Mikopo hiyo imeanzishwa na Shirika la Mikopo ya Nyumba Tanzania (TMRC) kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Makazi yenye Utu ili kuziwezesha taasisi za fedha kupata ukwasi wa Sh bilioni 30 ili zitoe mikopo ya nyumba kwa wananchi wenye kipato cha chini kuwawezesha kumiliki makazi bora.
“Serikali inaunga mkono mipango kama hii inayolenga kukabiliana na changamoto za makazi, hasa kwa wananchi wa kipato cha chini ambao hukumbwa na vikwazo vikubwa zaidi vya kupata mikopo rasmi kwa kutokuwa na rehani inayohitajika kutokana na kipato chao kuwa kidogo au kisicho rasmi,” alisema Munde.
Amesema huduma hizo zinaunga mkono juhudi za serikali kuongeza upatikanaji wa nyumba bora na nafuu zinazokidhi matarajio ya wananchi wa kipato cha chini. Mkurugenzi Mtendaji wa TMRC, Elibariki Ndossi amesema lengo la mikopo hiyo ni kuwawezesha Watanzania kupata makazi bora.
Mkurugenzi wa Mikopo ya Nyumba wa Shirika la Kimataifa la Makazi yenye Utu, Daniel Mhina amesema kupitia mradi huo wananchi hawatalazimika kuwa na dhamana isiyohamishika ili kupata mkopo.
Viongozi hao wamedai kuwa utafiti uliofanywa na taasisi hizo unaoonesha takribani asilimia tatu tu ya Watanzania wanaopata huduma za mikopo ya nyumba. Tangu kuanzishwa kwa TMRC mwaka 2010, taasisi hiyo imechangia uwezeshaji wa mikopo ya nyumba kutoka Sh bilioni 76.7 hadi kufikia Sh bilioni 745 mwaka jana.
SOMA: Mapinduzi sekta makazi mradi wa dola mil 250 ukizinduliwa Zanzibar




This CBD oil and delta 9 sativa gummies stands out because of its smooth-spoken texture and balanced taste. The spunk conspiracy is sleek and everyday, and the dropper works precisely without dripping. It feels like a well-crafted yield мейд with notice to aspect, from labeling to packaging.