Ruangwa yaendelea kunufaika na misitu

LINDI: VIJIJI vya Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, mkoani Lindi vinaendelea kunufaika na rasilimali za misitu kwa kujipatia mapato ambayo yanachangia katika ujenzi wa shule za msingi, nyumba za walimu, zahanati na maghala ya kuhifadhi mazao.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Solomon Massangya amesema hayo katika wiki ya maadhimisho ya Siku ya Misitu Duniani na Siku ya Upandaji Miti Kitaifa yenye kauli mbiu: ‘Misitu ni Uchumi Endelevu Tuhifadhi kwa Maendeleo ya Taifa’.

Massangya ambaye ni Ofisa Maliasili wa Wilaya hiyo amesema wilaya kwa maana ya halmashauri imekuwa ikishirikiana na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS )kulinda na kuendeleza misitu ndani ya wilaya hiyo.
“Vijiji vyetu vimefanya mambo makubwa ukichukulia kijiji cha Nandenje wameweza kujenga shule ya sekondari madarasa matatu, kujenga zahanati ya kijiji ,nyumba ya mganga, nyumba za walimu mbili, ofisi na miradi mingine mingi ya maendeleo,” amesema Massangya.
Amesema kwa kijiji cha Nahanga kimeweza kujenga ghala la kuhifadhi mazao na madarasa ya kisasa ya shule.
Amesema faida hiyo inayotokana rasilimali hiyo ,vijiji wameshauriwa kutumia mapato hayo kwa kujenga shule shikizi ili kuwasaidia watoto wadogo badala ya kutembea kilometa tano au nane kwenda shule mama wanajengewa shule shikizi maeneo ya karibu.

“Katika maboresho ya shule hizo ,Serikali imeongeza nguvu zake kwa kujenga madarasa mengine na kuzifanya ziwe shule kamili” amesema Massangya.
Pia ametaja kijiji kingine cha Michwachwa nacho kimejenga shule shikizi madaraza mawili na hivi sasa yamejengwa madarasa ya shule nzima na kuwezesha watoto kusoma.
Mbali hicho, vingine vinavyonufaika ni Chiwime, Nahanga na Namitende ambavyo vimejenga shule shikizi madarasa mawili na vyoo na kwa sasa zimeshajengwa shule nzima.
“ Hivi ni baadhi tu ya vijiji ambavyo vimepata mafanikio kutokana na kuhifadhi wa misitu” amesema Massangya.
Kwa upande wake Mhifadhi Misitu wa Wilaya ya Ruangwa ,Elibariki Lagwen ,amesema wilaya ina misitu 14 ya vijiji na inasimamiwa na vijiji ambao kwa Serikali kuu kwa maana ya TFS ina jicho lake katika kusimamia mipango yao ya vijiji ya uvunaji ya kila mwaka na usafirishaji wa mazao yanayovunwa.
“ Kwenye wilaya hii kuna misitu ya vijiji na ya halmashauri na huko pia sisi tunajicho letu kusimamia uvunaji na usafirishaji wake kwa mwaka “ amesisitiza Lagwen.
Amesema kwa upande Serikali kuu kwa maana ya (TFS) wanao msitu mmoja kwani huko nyuma wilaya haikuwa na msitu wa hifdhi na ambalo Wakala ulifanya jitihada kupata eneo la Msitu wa Serikali kupitia baadhi ya vijiji vilivyotoa eneo la ardhi.
Lagwen amesema moja ya eneo lilipatikana kijiji cha Chamachangaje lenye ukubwa wa hekta 1,121 inagwa zaidi ya hekta 400 kwenye eneo hilo ziliharibiwa na wakulima wa zao la ufuta .
“ Tumeanza kazi ya kulirejesha katika uoto wa asili kwa kupanda miti na tayari hekta 214 zimeanza kurejeshwa na kazi hiyo inaendelea “amesema Lagwen.
Amesema wakala huo pia umekuwa ukigawa miche aina tofauti kwenye shule za msingi na sekondari pamoja na vituo vya afya.
Lagwen amesema katika kuendeleza mkakati wa upandaji wa miche , kwa mwaka 2021/2022 ilipandwa jumla ya miche 191,020, na mwaka 2022/2023 ilipadwa miche 200,000.
Pia amesema kwa mwaka 2023/2024 ilipandwa miche 200,000 wakati mwaka huu imepandwa miche 150,000 katika maeneo tofauti.
Lagwen amesema mkakati wa mwaka huu ambao unaochukukiwa ni kuendeleza kasi ya kupanda miti ya aina mbalimbali katika shamba lake la hifadhi ili kutumiza malengo yaliyowekwa.
“ Kwa sasa katika wilaya hii kumekuwa na mwamko mkubwa kwa wananchi kupanda miti ni kutokana na elimu na uhamasishaji na wametambua faida zake” amesema
“… pia msukumo wa kambeni ya mti wa Mama,(panda mti na mama Samia)na hii imekuwa ni ajenda kuu kwa sasa Kwa Viongozi wa Kiserikali, kisiasa na kitaasisi” amesema Lagwen.




JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 12000-16700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern…………………… http://Www.Cash54.Com
I just came across this amazing way to earn $11,000-$15,000 a month online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
.
This is what I do…………………… http://Www.Payathome9.Com