Wananchi Shinyanga wanufaika mradi wa maji safi

SHINYANGA: WAKAZI zaidi ya 20,000 kutoka kata za Imesela na Bukene Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga wameanza kunufaika na mradi wa maji safi baada ya shirika lisilo la kiserikali la Water for Good kwa kushirikiana na Wakala wa Majisafi na Mazingira Vijijini (RUWASA) kutekeleza mradi wa usambazaji maji.

Hayo yamesemwa leo na Mhandisi wa Maji wa Shirika hilo, Raphael Lwassa walipokuwa wakikagua tenki la maji lenye ujanzo wa mita 100 lililojengwa kwenye kijiji cha Zumve kata ya Nyamalogo Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kwa lengo la kusukuma maji.

Mhandisi Lwassa amesema mradi umegharimu zaidi ya Sh bilioni 4.1 ikiwa ulianza utekelezaji mwaka 2024 nakutarajiwa kukamilila mwezi Disemba mwaka 2026.

Mhandis Lwassa amesema bomba la mtandao wa kilomita 44 limezamishwa kwaajili ya kusukuma maji kwa kutumia nishati ya jua kupeleka kwenye vijiji vitatu vya kata ya Bukene ambavyo ni Simbigu, Bukene na Masekelo

Mhandisi Lwassa amesema mradi huo kwa Kata ya Bukene unajumuisha kituo cha kusukuma maji kinachotumia nishati ya jua na tanki la kuhifadhi maji na vituo 31 vya kuchotea maji.

“Mradi unawafikia wakazi 11,668 kutoka kata ya Imesela na kutoka kata ya Bukene inawafikia wakazi 8,106 ambao wanapata maji safi na salama kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022″amesema Mhandisi Lwassa.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Water for Good Dave Levan amesema wamefurahi kutekeleza mradi kwa ushirikiano na kusisitiza kuendelea kutekeleza miradi mingine zaidi kwenye halmashauri kwaajili ya kusaidia wananchi na utunzaji wa mazingira.

Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Shinyanga Juliette Payovera amesema shirika hilo walianza kufanya nalo kazi mwaka 2021 kwa kutekeleza miradi ya maji kwenye maeneo mbalimbali ya halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Mhandisi Payovera amesema Mradi huu ambao ni usambazaji wa maji kwenye vijiji vinne ni awamu ya pili na wadau wametoa fedha kwa asilimia 62 na serikali kwa asilimia 28 na eneo limetolewa na wananchi wa kijiji cha Zumve.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro amesema mradi huo unatakiwa ulindwe na utunzwe kwani umesaidia wanawake na watoto kuondokana na adha ya kutembea umbali mrefu kutafuta maji ndoa zilivunjika na wanafunzi kukatiza masomo yao.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button