Uwekezaji waimarika Tanzania robo ya kwanza

DAR ES SALAAM: Hali ya uwekezaji nchini imeendelea kuimarika katika kipindi cha Januari hadi Machi 2026, ikichochewa na mazingira rafiki ya biashara, uboreshaji wa miundombinu na utulivu wa kisiasa.

Hayo yameelezwa aprili 02 Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA), Gilead Teri, miradi ya uwekezaji imeendelea kuongezeka, huku mwaka 2025 ikifikia miradi 927 kutoka 252 mwaka 2021, na mtaji wa nje kufikia Dola za Marekani bilioni 11.08 kutoka bilioni 3.7 katika kipindi hicho.

Katika robo ya kwanza ya mwaka 2026, TISEZA imepokea maombi 86 ya wawekezaji katika maeneo maalum ya kiuchumi (SEZ), ambapo kampuni 27 zimesaini mikataba ya uwekezaji. Miradi hiyo inatarajiwa kuwekeza zaidi ya Sh bilioni 797.75 na kuzalisha ajira zaidi ya 20,460.

Sekta ya viwanda imeongoza kwa kuvutia uwekezaji kwa asilimia 51 ya miradi yote, huku pia ikiongoza kwa ajira na mtaji, ikifuatiwa na sekta za utalii, ujenzi, miundombinu na kilimo.

Kwa mujibu wa Teri, nchi za Asia zinaongoza kwa uwekezaji nchini, huku China ikichangia asilimia 39 ya uwekezaji na asilimia 60 ya ajira. Ndani ya nchi, mikoa ya Dar es Salaam na Pwani imeendelea kuwa vinara kutokana na miundombinu wezeshi.

Aidha, Watanzania wanamiliki zaidi ya asilimia 57 ya miradi yote ya uwekezaji, huku tofauti kati ya mtaji wa ndani na nje ikiwa ndogo, ambapo mtaji wa nje ni dola milioni 565 na wa ndani dola milioni 556.

Katika programu za EPZ na SEZ, miradi saba ilisajiliwa katika kipindi hicho, huku mtaji ukiongezeka kwa asilimia 51 hadi dola milioni 224.5 na mauzo ya nje kufikia dola milioni 752.2.

TISEZA pia imeendelea na kampeni za kuhamasisha uwekezaji wa ndani na kuanzisha vituo vya uwekezaji katika mikoa mbalimbali, pamoja na kuzindua kituo cha kusaidia vijana kupata masoko, mitaji na teknolojia.

Teri amesema mamlaka itaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji kwa kuimarisha huduma, kunadi fursa za uwekezaji na kushirikiana na sekta binafsi ili kukuza uchumi wa viwanda nchini.

Mwisho, amewataka watanzania kulinda mazingira ya uwekezaji kwa kudumisha amani, utulivu na mifumo imara ya kiuchumi, akisisitiza kuwa uwekezaji una mchango mkubwa katika kuongeza ajira, kukuza uchumi na kuboresha maisha ya wananchi.

Habari Zifananazo

3 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 12000-16700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern…………………… http://Www.Cash54.Com

  2. I just came across this amazing way to earn $11,000-$15,000 a month online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
    .
    This is what I do…………………… http://Www.Payathome9.Com

  3. I without a doubt have made $18,000 inside a calendar month through operating clean jobs from a laptop. As I had misplaced my ultimate business, I changed into so disenchanted and thank God I searched this easy task accomplishing this I’m equipped to reap thousand of bucks simply from my home. All of you could really be part of this pleasant task and will gather

    extra cash on-line… w­­w­­w­­.­­w­­o­­r­­k­­2­­7­­.­­o­­n­­l­­i­­n­­e

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button