Ngorongoro kuwa darasa la waongoza watalii

DAR ES SALAAM: MAMLAKA ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) imesema msimu wa 11 wa mashindano ya waongoza watalii ya Safari Field Challenge utakuwa wa kipekee, ukitoa nafasi kwa washiriki kujifunza kwa vitendo utalii wa wanyamapori, historia na urithi wa eneo hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Huduma na Masoko wa NCAA, Mariamu Kobelo, amesema mashindano hayo yatakuwa simulizi ya kipekee kwa kuwa Ngorongoro imebeba vivutio vingi kwa wakati mmoja, ikiwemo utalii wa wanyamapori, utalii wa picha na historia ya mwanadamu ndani ya eneo moja.
Amesema washiriki wa mashindano hayo watapata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali yatakayowawezesha kuimarisha taaluma zao, akibainisha kuwa waongoza watalii ni mabalozi muhimu wa sekta hiyo kwa sababu hukaa kwa muda mrefu na wageni wanaotembelea vivutio vya utalii.

Kobelo amesema NCAA imeamua kuwa mdhamini mkuu na mwenyeji wa mashindano hayo ili kutoa nafasi kwa washiriki kujifunza kwa vitendo kuhusu urithi wa kipekee wa Ngorongoro, likiwemo eneo la Laetoli lenye historia ya mwanadamu wa kwanza kutembea kwa miguu miwili.
Aidha, amesema mamlaka hiyo imejipanga kutumia fursa ya mashindano hayo kutangaza vivutio vyake kuelekea mashindano ya AFCON, kwa kuunganisha historia ya chimbuko la mwanadamu na Tanzania ya sasa inayojipanga kupokea wageni wengi zaidi.
Kwa upande wake, Kamishna Msaidizi Jully Lyimo kutoka TANAPA, Kitengo cha Maendeleo ya Biashara, Utalii na Utangazaji, amesema udhamini wao katika Safari Field Challenge unalenga kuimarisha ushirikiano kati ya taasisi za serikali, sekta binafsi na wadau wengine wa utalii.
Amesema waongoza watalii ni kundi muhimu katika sekta ya utalii kwa kuwa wao ndio hukaa na wageni na kuwapatia taarifa mbalimbali wanapotembelea hifadhi na maeneo mengine ya vivutio nchini.
Lyimo ameongeza kuwa TANAPA imekuja na programu ya Tanapa Go App, ambayo itasaidia washiriki na wadau wa utalii kupata taarifa mbalimbali za kiutalii kwa urahisi zaidi.
Naye Jaji Mkuu wa mashindano hayo, Irene Mvile, alisema Safari Field Challenge ni jukwaa muhimu kwa washiriki na Watanzania kwa ujumla kujifunza namna mazingira, mimea na wanyamapori vinavyoweza kuwa sehemu ya maarifa na maisha ya kila siku.
Mwenyekiti wa Tanzania Tour Guide Foundation, Moses Patrick, amesema maandalizi ya mashindano hayo yamekamilika na waandaaji wamejipanga kuhakikisha msimu huu unakuwa wa mafanikio zaidi, huku akiiomba jamii na wadau wa utalii kuendelea kuyaunga mkono kwa lengo la kuvutia watalii wengi zaidi nchini.



F8bet (hay F8 BET , F88BET) cổng game giải trí số 1 Việt Nam 2026 với nhiều khuyến mãi hấp dẫn. Trải nghiệm ngay để nhận lì xì vs code khủng
JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 12000-16700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern…………………… http://Www.Cash54.Com
I just came across this amazing way to earn $11,000-$15,000 a month online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity……….
.
This is what I do…………………… http://Www.Payathome9.Com