Tume yazungumzia ushiriki wa vijana kutoa ushahidi
DAR ES SALAAM: MWENYEKITI wa Tume ya Kuchunguza Matukio ya Oktoba 29, Jaji Mkuu mstaafu, Mohamed Chande, amefafanua kuwa tume ilipokea maoni ya makundi mbalimbali, likiwemo kundi la vijana maarufu Gen Z, bodaboda, wamachinga, mamalishe na mengine kupitia jumuiya zao.
Kuhusu Gen Z, alisema walikutana nao katika ngazi mbalimbali ikiwemo kupitia Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu (TAHLISO).
“Wanafunzi wa vyuo vikuu wana serikali yao ya TAHLISO na mabunge yao. Tulikutana nao. Tena tuliwaambia waendeshe wenyewe mijadala, sisi tulikuwa wasikilizaji tu. Walitoa maelezo mazuri tu,” aliongeza.
Aidha, alizungumzia upotshaji ambapo alisema upotoshaji kuhusu tume ulianza tangu mwanzo kwa baadhi ya watu kutisha watoa ushahidi kuwa watatekwa, akasisitiza
“Upotoshaji wa aina hiyo unaumiza jamii. Tume inajitegemea asilimia 100. Watu wengi walitoa ushahidi kwa uhuru. Nikitaja idadi ya waliotoa ushahidi mtashangaa.”



