TESP yaimarisha mafunzo ya ualimu nchini

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo, amesema Serikali imepiga hatua kubwa katika kuimarisha mafunzo ya ualimu kupitia Mradi wa Kuendeleza Elimu ya Ualimu (TESP), uliolenga kuboresha ubora wa walimu na miundombinu katika vyuo vya ualimu 34 nchini.

Akizungumza jijini Dodoma wakati wa kikao cha kuhitimisha mradi huo, Prof. Nombo amesema TESP umefanikiwa kuingiza matumizi ya teknolojia katika ufundishaji kwa kuviunganisha vyuo na mkongo wa taifa, kujenga maabara, maktaba za kisasa pamoja na kuweka mifumo ya kidijitali inayorahisisha upatikanaji wa rasilimali za kujifunzia kwa wakufunzi na wanafunzi.

Amesema mradi huo pia umezingatia masuala ya ujumuishi na usawa wa kijinsia, huku ukitoa mafunzo ya uongozi kwa wakuu wa vyuo na watumishi ili kuhakikisha usimamizi bora wa mageuzi hayo. Aidha, amebainisha kuwa ujenzi wa miundombinu mipya umezingatia mabadiliko ya tabianchi, ikiwemo matumizi ya nishati mbadala na uhifadhi wa mazingira akitolea mfano Chuo cha Ualimu Kabaa.

Kwa upande wake, Mratibu wa mradi huo, Mwalimu Cosmas Mahenge amesema TESP umewekeza kwa kiasi kikubwa katika TEHAMA, vifaa vya kufundishia na kujifunzia pamoja na kuboresha mazingira ya vyuo. Hata hivyo, alieleza kuwa bado kuna haja ya kuimarisha zaidi usambazaji wa mtandao ndani ya majengo na kuwajengea uwezo wakufunzi ili kuendana na mitaala mipya ya mwaka 2023.

Naye Mkuu wa Chuo cha Ualimu Elimu Maalum Patandi, Mwalimu Lusiani Segesera, alisema chuo hicho kimenufaika kwa kupata maktaba, maabara za sayansi, vitabu pamoja na huduma ya mkongo wa taifa, hatua iliyoongeza ubora wa mafunzo na kutoa mwelekeo wa maendeleo ya baadaye.SOMA: Takukuru yaokoa vifaa vya mil 51/-ujenzi nyumba ya mwalimu

Mradi wa TESP ulitekelezwa kwa kipindi cha miaka nane tangu mwaka wa fedha 2017/18, ambapo Serikali ya Tanzania ilichangia takribani shilingi bilioni 140, huku washirika wa maendeleo kutoka Global Affairs Canada wakichangia bilioni 92. Serikali imesisitiza kuwa mafanikio ya mradi huo yataendelea kudumishwa hata baada ya kukamilika kwake.

 

Habari Zifananazo

One Comment

  1. Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…

    THIS→→→→ https://Www.FindJobs1.Site

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button