Nyalandu: Hatua zinazochukuliwa na Samia zitaiponya nchi

DAR ES SALAAM: SIKU chache baada ya Tume ya Rais ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 kuwasilisha ripoti yake, aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Lazaro Nyalandu amesema hatua zinazochukuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan zitasaidia kuwaunganisha Watanzania na kuiweka nchi salama.

Balozi Nyalandu, ambaye kwa sasa ni mshauri wa Masuala ya Diplomasia wa Rais Samia, amesema ahadi ya kutekelezwa kwa mapendekezo yaliyowasilishwa na Tume hiyo iliyokuwa chini ya Jaji Othman Chande, inatoa mwanga na taswira mpya ya kuliponya Taifa kutokana na kile kilichotokea Oktoba 29, 2025 wakati wa uchaguzi na baada.

Nyalandu amebainisha hayo hivi karibuni wakati akihojiwa na Televisheni ya Sky News ya nchini Uingereza kuhusu ripoti hiyo iliyowasilishwa na Tume.

SOMA: Jaji Chande azungumzia safari ya utendaji wa tume

,Balozi Nyalandu amesema Rais Samia ameahidi kuyafanyia kazi mapendekezo yaliyowasilishwa na Tume ya Jaji Chande huku baadhi akiyatolea maelekezo ya haraka ikiwemo ya majeruhi kupatiwa matibabu kwa gharama za Serikali.

Pia, amesema pendekezo na ahadi ya Rais Samia kuunda chombo cha kufuatilia kwa undani kuhusu matukio yaliyokwenda kinyume na wahusika kuwajibika, ni eneo ambalo linatoa tafsiri ya kuguswa na utayari wa kuijenga Tanzania mpya.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button