Madiwani Tandahimba wakumbushwa ukusanyaji mapato

MTWARA: MADIWANI wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara wamekumbushwa kuhakikisha wanahusika katika suala la ukusanyaji wa mapato kwenye kata zao ili kuleta maendeleo ya wananchi na halmashauri kwa ujumla.

Agizo hilo limetolewa katika Kikao cha Baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo kuhusu kupitia taarifa za utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwenye kata mbalimbali wilayani humo robo ya tatu kuanzia Januari hadi Machi kwa mwaka wa fedha 2025/2026.

Akizungumza wakati wa kikoa hicho, Mwakilishi kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkowa wa Mtwara, Edith Shayo amesema katika suala hilo la ukusanyaji wa mapato madiwani hao ndiyo wasimamizi wa mapato kwenye kata zao na kufanya hivyo itasaidia kuleta tija ya maendeleo kwenye halmashauri hiyo.

Mbali na hilo amewakumbusha kusoma kanuni ili kuleta uongozi bora huku akiwasisitiza wawe na mshikamano kwa kila kitu baina ya madiwani na wataalam wa halmashauri kwasababu wote wanajenga nyumba moja.

Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba, Kanali Michael Mntenjele amewataka vijana wa halmashauri hiyo kuchangamkia fursa zilizopo kwenye maeneo yao ikiwemo mikipo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri kupitia mapato yake ya ndani badala ya kutumia muda mwingi kukaa vijaweni pasipo kujishughulisha na shughuli za maendeleo.

‘’Wachangamkie fursa za ajira zinapojitokeza kwenye maeneo yao ikiwemo fursa za mikopo ya Rais Samia Suluhu Hassan hivyo waunde vikundi wafate taratibu watapata mikopo lakini muda mwingi  vijana wanakaa tu vijiweni kubeti badala ya kufanya shughuli za maendeleo’’amesema Mntenjele.

Naye Makamu Mwenyekiti wa kikao hicho ambaye pia ni diwani wa kata ya mahundo, Juma Ibrahim amesisitiza suala hilo la mshikamano baina yao na wataalam kwasababu watalaam ndiyo tegemeo la madiwani katika halmashauri hiyo kwenye masuala mbalimbali ikiwemo la maendeleo.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Tandahimba, Ahmed Katani amewaomba wataalam hao kuwa, wanapoona madiwani hao wanaleta hoja yoyote kwao inayohusu maslahi ya Tandahimba ni vema wakaifanyia kazi kikamilifu ili kuharakisha maendeleo.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. I found myself nodding along throughout this entire read. It makes you consider the nuances of the subject in a much clearer light. A truly insightful piece.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button