Serikali yatoa neno sheria ya elimu

Serikali imesema ipo kwenye mchakato wa kutengeneza sheria ya elimu ya mwaka 1978 baada ya kushirikisha wadau katika kutoa maoni yao ikiwemo adhabu ya viboko ambayo wamekuwa hawakubaliani nayo.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Mwakilishi wa Kamishna wa Elimu,Wizara ya Elimu sayansi na Teknolojia Mussa Mnyeti wakati akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Kukomesha Adhabu za Viboko, ambayo huadhimishwa April 30 ya kila mwaka.

Mnyeti amesema kuwa lengo la kutengeza sheria ambayo itaweza kumbeba kila mtu hivyo amewasisitiza wadau wote kutoka katika asasi za kiraia kusimama pamoja.

Awali akizungumza Mshauri wa Haki na Ulinzi wa Mtoto kutoka Shirika la Save the Children Wakili Barnabas Kaniki amesema kuwa adhabu za viboko kwa watoto zinaigharimu maisha.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji na Mratibu wa Kitaifa wa Chama cha wanawake wanaharakati wa Sheria na Maendeleo Afrika (WiLDAF Tanzania) Anna Kulaya pamoja Mkuu wa Idara ya
Utafiti, Ubunifu na Uchambuzi wa sera HakiElimu Makumba Mwemezi wamesema adhabu ya viboko inapoteza fursa kwa watoto na ubunifu.

Naye Mwalimu amesema ni vyema zikatumika mbinu mbadala za kumuadhibu mtoto na sio kumchapa huku pamoja na mwanafunzi akisema viboko zimekuwa vikisababisha wanafunzi kutoroka masomo shuleni.

Takwimu zinaonesha kuwa duniani kote, takribani watoto watatu kati ya wanne wenye umri wa miaka 2 hadi 14 hukumbana na aina fulani ya nidhamu ya ukatili majumbani huku Nchini Tanzania, watoto huripotiwa kukumbana na ukatili wa kimwili katika hatua mbalimbali za makuzi, huku walimu wakitajwa miongoni mwa wahusika katika mazingira ya shule.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu Wa Shirika la Jukwaa la Utu na Mtoto (CDF)Irene Ernest amesema adhabu ya viboko kwa wanafunzi inasababisha kutojiamini pindi wasomapo

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button