Kapinga awapa kipaumbele wazawa ajira viwandani

PWANI: Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga, amewashauri wamiliki wa viwanda vipya kutoa kipaumbele kwa wazawa kuhusu ajira ili kukuza uchumi na mapato ya taifa kwa ujumla.

Akizungumza Mei 09, 2026, wakati wa akifungua wa kiwanda kipya cha kutengeneza tambi cha Kura Food mkoani Pwani, Kapinga amesema serikali inaendelea kuboresha mazingira ya biashara ikiwemo sera, miundombinu, na mifumo ili kuvutia wawekezaji na wafanyabiashara na kuongeza ushindani wa bidhaa za Tanzania kimataifa.

Aidha, Wizara imefanya mapitio ya sheria na kanuni ili kuhakikisha zinajielekeza katika kuwezesha biashara na kuondoa vikwazo badala ya kudhibiti pekee. Lengo ni kushirikiana na wadau wa mnyororo wa thamani, kutumia teknolojia za kisasa zinazoongeza tija, uzalishaji, na ufanisi wa biashara nchini.

Naye, Mwenyekiti wa Kura Food, Wu Yeping, ameipongeza Serikali kwa kuweka mazingira rafiki yanayorahisisha uwekezaji.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge, amebainisha kuanza kwa uboreshaji wa miundombinu ya barabara na Reli ya Kisasa (SGR) kuanzia mwaka ujao ili kufungua zaidi fursa za kibiashara mkoani humo.

Naye, Mbunge wa Kisarawe, Selemani Jafo, amemshukuru Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwa sera zake thabiti ambazo zimekuwa chachu ya kuvutia wawekezaji. Sera hizi zimesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza changamoto ya ukosefu wa ajira kwa wananchi wa jimbo hilo kupitia kuanzishwa kwa viwanda vipya. 

Habari Zifananazo

One Comment

  1. I started this as a simple side hustle, and last month I made a little over $6,137 just working a few hours a day from my phone. If you want to check out how it works, the website has all the details.
    Here—>> http://www.giftpay7.vip

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button