Serikali yaweka maono ya kuibadili DITF ifikapo 2050

DAR ES SALAAM: Makamu wa Rais wa Emmanuel Nchimbi amesema maono ya Serikali ni kuona Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (DITF) yakibadilika kutoka eneo la kuonesha bidhaa pekee na kuwa kitovu cha ubunifu, utafiti, teknolojia na biashara za kimataifa ifikapo mwaka 2050.

Akizungumza katika kilele cha Jubilee ya Dhahabu ya miaka 50 ya Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba), Makamu wa Rais alisema maonesho hayo yanapaswa kuwa mahali pa kuwaunganisha wawekezaji, wabunifu na wajasiriamali, pamoja na kuzindua bidhaa mpya za Tanzania kwa ajili ya soko la dunia.

Amesema ili kufanikisha maono hayo, ni muhimu kuendelea kuimarisha mazingira ya biashara na kuhakikisha viwanda vinapata mitaji ya kutosha, akizitaka taasisi za fedha kuongeza mikopo kwa viwanda vidogo na vya kati kwa masharti nafuu yatakayowawezesha wafanyabiashara wengi zaidi kukuza uzalishaji.

Awali akizungumza na Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga alisema mauzo ya bidhaa na huduma za Tanzania nje ya nchi yameongezeka kwa kiwango kikubwa huku mauzo ya nje yakifikia takribani Dola za Marekani bilioni 18.6 huku mauzo ya bidhaa yakifikia Dola za Marekani bilioni 11 yakionesha ongezeko la asilimia 11.

Kwa Upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade)Dk, Latipha Mohamed Khamis amesema maadhimisho ya Miaka 50 ya maonesho hayo tokea kuanzishwa kwake yamezalisha Fursa za kibiashara na uwekezaji zenye thamani ya Takribani Sh trilioni 129.31 hivyo kuchangia kwa kiwango mikubwa cha ukuaji wa uchumi wa taifa.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button