Ndejembi achukizwa mradi wa umeme kukwama Kigoma

KIGOMA: Waziri wa Nishati, Deogratius Ndejembi ameeleza kutoridhishwa na utekelezaji wa mradi wa kuzalisha umeme katika Mto Malagarasi Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma unaotekelezwa na kampuni ya DONGFANG Electric International Corporationo (DEC).

Pia ameagiza kuondolewa eneo la mradi kwa mhandisi mkazi wa kampuni hiyo ayesimamia mradi huo Duan Longhai.

Waziri Ndejembi ametoa agizo hilo leo Mei 10, 2016 alipofanya ziara ya kutembelea na kukagua mradi huo ambapo amesema kuwa haridhishwi na hatua ya utekelezaji wa mradi ulipofikia ukilinganisha na kiwango cha pesa cha Dola milioni 20 ambacho tayari kampuni hiyo imepewa.

Ndejembi alisema kuwa pamoja na kutoa maagizo ya kuondolewa kwa mhandisi huyo pia amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO kufanya ukaguzi wa kazi ambazo zimeshatekelezwa hadi sasa ukilinganisha na pesa ambayo imeshatumika akitoa wiki mbili kwa kazi hiyo kufanyika na taarifa kuwasilishwa kwake.

“Tulichogundua hii kampuni haina uwezo na ilipata kazi hii baada ya kuomba kazi hii kwa gharama za chini kuliko waombaji wengine, hivyo tutaongea na Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki ili aongee na Balozi wa China tupate taarifa kazi ya uwezo wa kampuni hiyo na kazi ambazo wameshafanya ili tuone hatua za kuchukua,”alisema Waziri Ndejembi.

Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Razalo Twange alisema kuwa kwa sasa mkandarasi huyo yupo nyuma ya utekelezaji wa mkataba wake kwa asilimia 20 akiwa hajafanya kazi muhimu zikiwemo za ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami kilometa 27 kuelekea eneo la mradi, nyumba ya kuzalisha umeme (Power house) na nyumba za watumishi.

Alisema kuwa mradi huo wenye gharama ya zaidi ya Sh bilioni 370 tayari Mkandarasi kampuni ya DongFang Electrical International Corporation imeshalipwa dola milioni 20 za marekani kwa kazi hizo ambazo zilipaswa kuwa zimekamilika lakini miezi tisa sasa kazi hizo bado hazijafika hata nusu na TANESCO imefanya jitihada mbalimbali kukabiliana na changamoto hizo ikiwemo kukutana na mamlaka za juu za uongozi wa kampuni hiyo.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. I get paid more than $120 to $130 per hour for working online. I heard about this job 3 months ago and after joining this i have earned easily $15k from this without having online working skills.
    This is what I do…..    https://www.work27.info

  2. Google pays $95 on a regular basis. My latest salary check was $8200 for working 10 hours a week on the internet. My younger sibling has been averaging $15k for the last few months, and he constantly works approximately 24 hours. I’m not sure how simple it was once I checked it out. This is my main concern… GOOD LUCK…. http://www.giftpay7.vip

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button