Mfumo wa PRIS kuzinduliwa kesho

Dar es Salaam – Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania, Fatma Abdallah amesema Kampuni hiyo inaunga mkono Mfumo wa Kimkakati wa Uchumi wa Dijitali Tanzania (2024–2034), unaolenga kuiweka nchi kama kitovu cha kidijitali cha kikanda kwa kuimarisha miundombinu, kupanua ujumuishaji wa kifedha, na kuendesha ukuaji wa uchumi.

Hayo ameyasema Leo jijini Dar es salaam wakati alipokutana na waandishi wa habari akiwapitisha kwenye mafunzo ya mfumo wa Programu ya PRIS App ya Puma Energy ambapo utazinduliwa kesho wenye lengo la kurudisha kwa wateja wao.

Aidha Abdallah amesema Kampuni inanaendesha zaidi ya vituo 2201 vya rejareja na kuhudumia viwanja 107 vya ndege duniani. Lengo letu ni kuhamasisha jamii ili kuendeleza ukuaji na mafanikio. Ikiwa na mpango kufika mwaka 2030 idadi yake itakuwa maradufu kwa lengo la kukuza uchumi wa Nchi.

Amesema kwa miaka mitatu iliyopita pekee, Puma Energy Tanzania imechangia zaidi ya TZS trilioni 1.4 kwa Serikali kupitia kodi na ushuru. Mwaka 2025, kampuni ilitangaza gawio la TZS bilioni 21, likiimarisha mapato ya kifedha yanayotokana na umiliki wa Serikali wa 50% kupitia Msajili wa Hazina. Kufuatia kuzinduliwa kwa mafanikio katika nchini za Zimbabwe (Novemba 2025), Malawi (Februari 2026), na Botswana (Machi 2026), Tanzania inakuwa soko la nne barani Afrika.

Mkurugenzi Mtendaji huyo amebainisha kuwa Kampuni hiyo inahudumia mafuta kwenye ndege hapa Nchini viwanja nane huku vya kimataifa vitatu na kitaifa nane na kusema kuwa mafuta yapo ya kutosha kuhudumia Watanzania.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button