Serikali kujizatiti mazingira bora uwekezaji

DAR ES SALAAM: NAIBU Waziri wa Nishati, Salome Makamba amesema Serikali itaendelea kuweka mazingira bora kwa wawekezaji katika usafirishaji, viwanda kilimo na huduma mbalimbali ili sekta hiyo Ibaki imara katika ushindani na manufaa kwa wananchi.
Akizungumza Dar es Salaam kwenye uzinduzi wa Mfumo wa Pris App Puma Energy, Makamba amesema sekta ya nishati ni injini ya uchumi inayowezesha ukuaji wa uchumi nchini kupitia upanuzi wa vituo vya usambazaji na uwekezaji wa nishati safi na ubunifu wa kidijitali.
Aidha, Salome amesema uzinduzi wa Mfumo huo unaenda moja kwa Moja na malengo ya Digital Economy Strategic Framework(DESF) 2024-2034 ambayo inalenga kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha uchumi wa kidijitali Afrika.

Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania, Fatma Abdallah amesema programh hiyo inaunga mkono dira ya taifa ya uchumi wa kidijitali na wao kama Kampuni ni mshirika katika Sekta ya nishati hivyo kusukuma mbele gurudumu hilo.
Aidha, Fatma amesema maendeleo hayajengwi kwa kuuza bidhaa na kutoa huduma pekee bali kujenga thamani ,ubunifu na kuimarisha mahusiano ya muda mrefu na jamii wanayoihudumia.



