Hivi hapa vipaumbele Ardhi bajeti 2026/27

DODOMA; Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imepanga kutekeleza vipaumbele vinane katika mwaka wa fedha 2026/27.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Leonard Akwilapo, leo Mei 28, 2028 akiwasilisha hotuba ya bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka 2026/27.

Amevitaja vipaumbele hivyo kuwa ni kuongeza kasi ya upangaji, upimaji, umilikishaji na usajili wa ardhi mijini, vijijini na maeneo ya kimkakati.

Vingine ni kuandaa mipango ya matumizi ya ardhi ya vijiji, kuimarisha mifumo ya TEHAMA katika utunzaji wa kumbukumbu, utoaji wa huduma, ukusanyaji wa maduhuli na upatikanaji wa taarifa za ardhi na uthamini.

“Kuimarisha mifumo ya utatuzi wa migogoro ya ardhi kwenye Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya, kuhakikisha uwepo wa nyumba bora, ukuaji wa sekta ya milki na maendeleo ya makazi kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii;

“Kuimarisha mipaka ya Kimataifa na kuendeleza miji ya mipakani, kuimarisha upatikanaji wa ramani ili kuwezesha uandaaji wa mipango ya Kitaifa na matumizi mengine; na kuimarisha mifumo ya usimamizi na ufuatiliaji wa utekelezaji wa vipaumbele,” amesema Waziri.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button