Filamu ya kuhamamisha utalii kuachiwa Juni 21

DAR ES SALAAM: Kampuni ya Kitanzania ya Ngoteya Wild, imetangaza kuwa filamu mpya ya ‘Sentinels of Engaruka’ ambayo wamefanya kwa kushirikiana na African people and wildlife itaoneshwa rasmi kupitia Juni 21. 2026 kupitia Youtube.

Filamu hiyo imechukua zaidi ya miaka mitatu kuandaliwa, ikihusisha utafiti wa kina, upigaji picha wa mazingira ya asili na simulizi inayoonesha uhusiano wa kipekee kati ya jamii ya Kimasai, twiga na mazingira ya Engaruka mkoani Arusha.

Toleo la Kiswahili la filamu hiyo limesimuliwa na mtangazaji maarufu Meena Ally, ambaye sauti yake itaongeza mguso wa kipekee katika kuifikisha hadithi hiyo kwa watazamaji wa Tanzania na Afrika Mashariki.

Kwa mujibu wa Hans Ngoteya, filamu hiyo inalenga kuhamasisha uhifadhi wa maliasili, kuonesha utajiri wa urithi wa Tanzania na kuifikisha hadithi ya Engaruka kwa hadhira ya kimataifa kupitia jukwaa la YouTube.

Sentinels of Engaruka ni moja ya miradi mikubwa ya filamu za uhifadhi iliyotayarishwa nchini Tanzania, ikiwa na lengo la kuonesha namna jamii na wanyamapori wanavyoweza kuishi kwa maelewano huku wakilinda mazingira kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button