Prof Kitila: Dira 2050 kufanikisha maendeleo endelevu

New York, Marekani: Tanzania imesema utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 utaongeza kasi ya kufikiwa kwa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) kwa kuyajumuisha kikamilifu katika mipango ya muda mfupi, wa kati na wa muda mrefu wa maendeleo ya nchi.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, Prof Kitila Alexander Mkumbo Julai 13, 2026 alipohutubia Mdahalo Mkuu wa Jukwaa la Kisiasa la Ngazi ya Juu la Umoja wa Mataifa la Maendeleo Endelevu (High-Level Political Forum – HLPF) unaoendelea New York, Marekani.
Akiwasilisha tamko la Tanzania katika mdahalo huo, Prof Mkumbo ameeleza kuwa, pamoja na changamoto zinazoikabili dunia, zikihusisaha mabadiliko ya tabianchi, misukosuko ya uchumi na migogoro ya kikanda, Tanzania imeendelea kupata mafanikio katika utekelezaji wa SDGs.
“Tumeongeza upatikanaji na huduma za maji safi na usafi wa mazingira, kuimarika kwa huduma za afya, kupanuka kwa fursa za elimu bora, kuongezeka kwa upatikanaji wa umeme, kuharakishwa kwa mageuzi ya kidijitali, uwekezaji katika miundombinu ya kimkakati, pamoja na kuimarika kwa uhamasishaji wa rasilimali za ndani na uwezo wa taasisi za umma,” amesema.
Prof Mkumbo ameongeza kuwa Tanzania inaona Agenda 2030 ikiwa sehemu ya safari ya maendeleo ya muda mrefu, ikifungamanishwa na utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 kupitia Mpango wa Nne wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano (FYDP IV), kwa pamoja inaweka msingi wa kuendeleza utekelezaji wa SDGs hata baada ya mwaka 2030.
Alifafanua kuwa, vipaumbele vya utekelezaji katika kipindi kijacho ni pamoja na kilimo cha kisasa, maendeleo ya viwanda, uchumi wa buluu, kuimarisha ustahimilivu dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, mageuzi ya kidijitali, maendeleo ya rasilimali watu na uhamasishaji wa rasilimali za ndani ili kuchochea ukuaji jumuishi na endelevu.
Aidha, Waziri amesisitiza kuwa pamoja na dhamira ya Serikali, mafanikio ya Ajenda 2030 yanategemea ushirikiano madhubuti wa kimataifa, ukizingatia kuwa nchi nyingi zinazoendelea bado zinakabiliwa na nakisi ya kibajeti inayopunguza kasi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Ametoa wito kwa Jumuiya ya Kimataifa kutekeleza kikamilifu Azimio la Siasa la Umoja wa Mataifa la mwaka 2023 na kuunga mkono mpango wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa SDG Stimulus, ikiwemo kupunguza riba za mikopo, kushughulikia changamoto za madeni, kuongeza upatikanaji wa mikopo nafuu ya kugharamia miradi ya maendeleo na kuharakisha mageuzi ya mfumo wa fedha wa kimataifa ili uwe jumuishi na unaozijali zaidi nchi zinazoendelea.
Baadaye leo, Julai 14, 2026, Tanzania itawasilisha rasmi taarifa yake ya Tatu ya Mapitio ya Hiari ya Nchi ya Utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (Third Voluntary National Review VNR).




F8BET thương hiệu giải trí cùng worl cup 2026