MUST yatakiwa kuwa kinara wa teknolojia

RUKWA:Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Mbeya (MUST) kimetakiwa kuelekeza nguvu zaidi katika tafiti, ubunifu na matumizi ya teknolojia zinazolenga kutatua changamoto za maendeleo nchini, ili kiwe kinara wa sayansi na teknolojia katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda, amesema hayo Oktoba 11, 2026, alipotembelea Kampasi ya MUST Rukwa iliyopo eneo la Kianda, mkoani Rukwa, akisisitiza umuhimu wa chuo hicho kutekeleza jukumu lake la kuendeleza sayansi na teknolojia kwa manufaa ya taifa.

Amesema MUST inapaswa kuwekeza katika teknolojia za kisasa na ubunifu unaojibu mahitaji ya Tanzania, akitolea mfano wa roboti, ndege zisizo na rubani, teknolojia za kilimo na uhandisi, huku akisisitiza umuhimu wa kujenga uwezo wa ndani wa kubuni na kuzalisha teknolojia hizo.
Profesa Mkenda amesema ili kufikia azma hiyo, chuo hicho kinapaswa kuimarisha ushirikiano na taasisi za elimu ya juu na vyuo vya sayansi na teknolojia ndani na nje ya nchi kupitia programu za kubadilishana wanafunzi na watumishi, tafiti za pamoja pamoja na kubadilishana ujuzi na uzoefu wa kitaalamu.
Aidha, ameeleza kuwa serikali inatarajia kuona MUST ikiimarisha uhusiano na vyuo vya nchi mbalimbali, zikiwemo China, Belarus na Uturuki, ili kuongeza fursa za mafunzo, tafiti na uendelezaji wa teknolojia.

Amesisitiza kuwa mafanikio ya MUST hayatapimwa kwa idadi ya wanafunzi pekee, bali pia kwa ubora wa wahitimu, tafiti zinazofanyika, ubunifu unaozalishwa na teknolojia zinazoweza kutumika kutatua changamoto za jamii.
Akizungumza baada ya ziara hiyo, Makamu Mkuu wa MUST, Profesa Aloys Mvuma, ameahidi kutafsiri maono na malengo ya Serikali kwa vitendo, akisema chuo hicho kinaendelea kujiandaa na kuweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha malengo ya kuendeleza sayansi na teknolojia yanafikiwa.

Kampasi ya MUST Rukwa inatoa programu za Uhandisi Umeme, Uhandisi Mitambo, Kilimo na Biashara katika ngazi za stashahada na shahada.




Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…
THIS→→→→ http://Www.Payathome1.com