Mwenge wazindua miradi ya maendeleo Kwela

RUKWA; Mwenge wa Uhuru umeendelea kuwa chachu ya maendeleo nchini baada ya kumulika na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo katika Jimbo la Kwela, Wilaya ya Sumbawanga, mkoani Rukwa, huku viongozi wakisisitiza umuhimu wa kulinda amani kama msingi wa utekelezaji shughuli za maendeleo.
Mbio hizo za Mwenge wa Uhuru zilifika Kata ya Laela na kuzindua miradi inayohusisha sekta za elimu, afya na miundombinu, ikiwemo shule ya sekondari, zahanati na daraja, sambamba na shughuli za ujenzi wa barabara.

Akizungumza katika Kata ya Laela, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Wazo Mwang’onda, amesema utekelezaji wa miradi hiyo ni miongoni mwa matokeo ya mazingira ya amani iliyopo nchini.
Amewataka wananchi wa Mkoa wa Rukwa kuendelea kuitunza na kuilinda amani, akisisitiza kuwa maendeleo endelevu yanahitaji utulivu, ushirikiano na mshikamano miongoni mwa wananchi.
Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Kwela ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Sangu, ameishukuru Serikali inayoongozwa na Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kupeleka miradi ya maendeleo katika Mkoa wa Rukwa, hususan Jimbo la Kwela.

Sangu amesema miradi iliyozinduliwa na Mwenge wa Uhuru ina umuhimu mkubwa kwa wananchi wa jimbo hilo, akieleza kuwa utekelezaji wake unatarajiwa kuboresha huduma za kijamii na kuchochea maendeleo ya eneo hilo.
Pia Waziri Sangu ameupongeza Mfuko wa Taifa wa Hifadhi wa Jamii (NSSF) kwa kuendelea kuyafikia makundi mbalimbali ya vijana waliojiari wakiwemo madereva boda boda zaidi ya 1900, ambapo NSSF iliwapa elimu ya hifadhi ya jamii na kuwasajili kuwa wanachama kupitia mpango wa Hifadhi Skimu.




C168 là nhà cái trực tuyến với kho game đa dạng từ casino, thể thao, bắn cá đến nổ hũ. Khám phá giao diện hiện đại, nhiều ưu đãi và tiện ích dành cho thành viên.