Ajali ya lori yaua dereva Tanga

TANGA; Dereva Ponsiano Taabuya amefariki dunia kufuatia ajali ya barabarani iliyotokana na lori la mizigo kupinduka na kusababisha kifo cha dereva huyo eneo la Muheza–Kibanda, Wilaya ya Muheza, mkoani Tanga.

Kulingana na taarifa kwa umma iliyotolewa leo Oktoba 11, 2026 na Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, ajali hiyo ilitokea  Oktoba 10, 2026 majira ya saa 11 jioni.

Ajali hiyo ilihusisha gari la lori la mizigo lenye namba za usajili T.491 EFD, lililokuwa limeunganishwa na tela zenye namba T.582 EEZ na T.384 DTY likitokea jijini Tanga kuelekea nchini Zambia.

Taarifa imesema uchunguzi wa awali unaonesha dereva Ponsiano alishindwa kulimudu gari hilo hatua iliyosababisha kupinduka.

Matokeo ya uchunguzi wa awali yanaonesha kuwa chanzo cha ajali hiyo kinadhaniwa ni dereva kushindwa kulimudu gari hilo, hatua iliyosababisha kuacha njia na kupinduka.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button