Serikali, ZLS zakubaliana kuimarisha huduma za msaada wa kisheria

ZANZIBAR: Chama cha Mawakili Zanzibar (ZLS) na Wizara ya Ofisi ya Rais – Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora wamekubaliana kuimarisha ushirikiano katika utoaji wa huduma za msaada wa kisheria kwa wananchi, pamoja na kufanya mapitio na marekebisho ya sheria mbalimbali.
Makubaliano hayo yalijadiliwa wakati wajumbe wa Baraza la Uongozi la ZLS walipotembelea ofisi za wizara hiyo na kukutana na Waziri mwenye dhamana ya wizara hiyo, Dk Haroun Ali Suleiman. Ziara hiyo ililenga kuimarisha mahusiano ya kiutendaji kati ya taasisi hizo.
Ujumbe wa ZLS uliongozwa na wajumbe wa Baraza la Uongozi, Masoud Salim, Alphonce Gura na Mufida Salum, ukiambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa chama hicho, Shabani Seleman Mwangoda.
Akizungumza katika kikao hicho, Mwangoda amesema ZLS inaendelea kuboresha mifumo yake ya utendaji na iko tayari kushirikiana na Idara ya Msaada wa Kisheria ya wizara hiyo ili kupanua upatikanaji wa huduma hizo kwa wananchi wote wa Zanzibar.
Ameongeza kuwa chama hicho kimejipanga kuanzisha mfumo wa kidijitali utakaowawezesha wananchi kuomba huduma za msaada wa kisheria kupitia tovuti ya ZLS, www.zls.or.tz.
Kwa upande wake, Dk Haroun ameipongeza ZLS kwa juhudi zake za kuimarisha ushirikiano na wizara, huku akisisitiza umuhimu wa kukishirikisha chama hicho zaidi katika shughuli mbalimbali za wizara.
Amesema huduma za msaada wa kisheria zina nafasi muhimu katika kuwafikia wananchi wenye uhitaji na kuchangia maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kisiasa.

“Ninasisitiza ushirikiano wa karibu zaidi na Chama cha Mawakili kwa kuongeza ushirikishwaji wao katika shughuli mbalimbali za Wizara,” amesema Dk Haroun.
Naye Mkurugenzi wa Katiba na Huduma ya Msaada wa Kisheria wa wizara hiyo, Hanifa Ramadhani, ameahidi kuimarisha ushirikiano na ZLS katika maeneo yaliyokubaliwa. Amesema hatua hiyo itajumuisha kufufua juhudi za kuandaa Hati ya Makubaliano (MoU) kati ya taasisi hizo ili kurahisisha utekelezaji wa majukumu yao ya pamoja.
Wajumbe wa Baraza la Uongozi la ZLS pia wameeleza utayari wao wa kushirikiana na wizara katika kufanya mapitio na marekebisho ya sheria mbalimbali.
Aidha, wajumbe hao wamemualika Dk Haroun kushiriki Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Mawakili Afrika Mashariki (EALS), unaotarajiwa kufanyika Zanzibar mwezi Novemba 2026, ambapo ZLS itakuwa mwenyeji.
Katika kuhitimisha ziara hiyo, Dk Haroun alimkabidhi Mwangoda nakala ya Sera Mpya ya Msaada wa Kisheria ya mwaka 2026, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha uelewa na ushirikiano katika utekelezaji wa huduma hizo.




Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…
THIS→→→→ http://Www.Payathome1.com