Posta yaimarisha usalama viwango vya kimataifa

CHAD: Shirika la Posta Tanzania (TPC) limejiunga na nchi nyingine za Afrika katika mafunzo ya viwango vya kimataifa vya usalama wa huduma za posta, yanayolenga kudhibiti hatari katika usafirishaji wa nyaraka na vifurushi.

Mafunzo hayo ya viwango vya S58 na S59 vya Umoja wa Posta Duniani (UPU) yamefanyika jijini N’Djamena, Chad, kuanzia Novemba 10 hadi 12, 2026, yakishirikisha wawakilishi kutoka takribani nchi 30 za Afrika.

Tanzania imewakilishwa na Mkuu wa Kitengo cha Mambo ya Ndani wa Shirika la Posta, Mathias Kipeta, pamoja na wataalamu wengine wa sekta hiyo kutoka mataifa mbalimbali.

Viwango vya S58 na S59 vinaweka matakwa ya kiusalama katika shughuli za posta, ikiwemo ulinzi wa vituo vya usafirishaji na udhibiti wa mifumo inayohusika na utunzaji na usafirishaji wa barua na vifurushi.

Kupitia mafunzo hayo, wataalamu wanapata fursa ya kubadilishana uzoefu kuhusu namna ya kutekeleza viwango hivyo na kukabiliana na changamoto za kiusalama zinazoweza kuathiri usafirishaji wa mizigo ya posta.

Utekelezaji wa viwango hivyo ni sehemu ya juhudi za kuimarisha usalama wa mtandao wa posta, kulinda mizigo ya wateja na kujenga imani katika huduma zinazotolewa na mashirika ya posta barani Afrika.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button