Wanafunzi vyuo vya uuguzi kupimwa selimundu

DAR ES SALAAM; Wanafunzi wa vyuo vya uuguzi na ukunga nchini wanatarajiwa kupimwa vinasaba vya ugonjwa wa selimundu katika kampeni ya kitaifa ijulikanayo kama ‘Vunja Mduara’ inayolenga kuongeza uelewa, kuwajengea uwezo wa kujitambua na kuvunja mnyororo wa kurithishwa kwa ugonjwa huo kutoka kizazi kimoja kwenda kingine.
Kampeni hiyo imezinduliwa rasmi Novemba 14, mwaka huu katika Chuo Kikuu cha Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS)jijini Dar es Salaam, kwa ushirikiano wa Wizara ya Afya, Chama cha Wakunga na Wauguzi Tanzania(TANNA), Chama cha Wanafunzi wa Ukunga na Uuguzi Tanzania (UNSATA) na Tanzania Sickle Cell Disease Alliance.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Tiba na Uuguzi wa Wizara ya Afya, Paul Magesa amesema serikali imeona umuhimu wa kuanza na wanafunzi wa uuguzi, ukunga na taaluma nyingine za afya ili wawe mfano katika kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kupima vinasaba vya selimundu.
Amesema kampeni hiyo inalenga kuhakikisha wananchi wanajitambua mapema hali zao za kinasaba, ili waweze kufanya maamuzi sahihi kuhusu afya ya uzazi na kupunguza uwezekano wa kupata watoto wenye ugonjwa huo.
“Pale wazazi wote wawili wanapokuwa na vinasaba vya selimundu, wanakuwa na uwezekano wa asilimia 25 kupata mtoto mwenye ugonjwa huo, asilimia 50 kupata mtoto mwenye vinasaba na asilimia 25 kupata mtoto asiye na vinasaba hivyo.
Amesema kutokana na hali hiyo, upimaji ni hatua muhimu katika kuzuia kuendelea kwa mnyororo wa kurithisha ugonjwa huo, akisisitiza kuwa jamii inapaswa kutumia huduma zinazopatikana katika vituo vya kutolea huduma za afya kujua hali zao za kinasaba.

Ameongeza kuwa matibabu ya ugonjwa wa selimundu yana gharama kubwa, ambapo makadirio ya gharama za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja kwa mgonjwa mmoja yanaweza kufikia Sh milioni 70, hivyo kuzuia ugonjwa huo ni muhimu kuliko kusubiri wagonjwa wengi waongezeke.
“Serikali kupitia Hospitali ya Benjamin Mkapa inatoa huduma ya upandikizaji wa uroto kwa baadhi ya wagonjwa wa selimundu, ambayo ni miongoni mwa tiba zinazoweza kuponya ugonjwa huo, lakini gharama zake ni kubwa.
Kwa upande wake, Rais wa TANNA , Dk Ezekiel Henry amesema kampeni ya ‘Vunja Mduara’ ni mpango muhimu unaolenga kuzuia kuendelea kuzaliwa kwa watoto wenye ugonjwa wa selimundu kupitia elimu na upimaji wa vinasaba kwa vijana.
Amesema wameanza na wanafunzi wa vyuo vya kati na vikuu kwa kuwa wapo katika umri ambao wengi wao wanaanza kufanya maamuzi kuhusu mahusiano ya kudumu na kuanzisha familia, hivyo ni muhimu wafahamu hali zao za kinasaba mapema.
Dk Ezekiel amesema kampeni hiyo itaendelea katika vyuo vya kati na vikuu nchini kote kwa lengo la kuwafikia wanafunzi wengi zaidi na kuwapa elimu itakayowawezesha kufanya maamuzi sahihi kuhusu afya zao na familia wanazotarajia kuanzisha.
Amesema TANNA kitatumia mtandao wake wa matawi 59 yaliyopo nchini pamoja na matawi madogo zaidi ya 185 kusambaza elimu ya selimundu kwa wananchi na kuhakikisha ujumbe wa kampeni hiyo unafika katika maeneo mbalimbali.




NEW88 – Nhà Cái Giải Trí Trực Tuyến Hàng Đầu, Mang Đến Trải Nghiệm Cá Cược Đẳng Cấp Với Kho Game Đa Dạng tham gia tại: https://new881c.com/
NEW88 – Nhà Cái Giải Trí Trực Tuyến Hàng Đầu, Mang Đến Trải Nghiệm Cá Cược Đẳng Cấp Với Kho Game Đa Dạng tại: https://revistabienestar.com.co