“Huduma bora mama, mtoto ziwafikie wote”

DAR ES SALAAM. Rais Dk Samia Suluhu Hassan, amesema huduma bora za mama na mtoto zinapaswa kuwafikia wanawake na watoto kulingana na mahitaji yao, hasa katika maeneo yenye upungufu mkubwa wa huduma.
Dk Samia amesema hayo akielezea kufurahishwa kwake na kaulimbiu ya Mkutano wa Tatu wa Kitaifa wa Kisayansi kuhusu Afya ya Uzazi, Mama, Mtoto Mchanga, Mtoto, Vijana na Lishe.
“Niseme nimefurahishwa na kaulimbiu ya mkutano huu, isemayo: Kuharakisha Matokeo yenye Usawa ya Huduma za Mama na Mtoto kupitia Ugharamiaji Endelevu, Ubunifu katika Kutatua Changamoto, na Mifumo Imara ya Afya nchini Tanzania.



