Gomez, Pluijm wang’ara Januari

BRUNO Gomez wa timu ya soka ya Singida Big Star,  amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Januari wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa mwaka 2022/23, huku Kocha Mkuu wa timu hiyo, Hans Pluijm akichomoza Kocha Bora wa mwezi huo.

Taarifa ya Bodi ya Ligi (TPLB), imesema Kikao cha Kamati ya Tuzo kilichokutana wiki hii kilimteua Gomez, baada ya kuonesha kiwango kizuri kwa mwezi Januari na kutoa mchango mkubwa kwa Singida, ikiwa ni pamoja na kufunga mabao mawili na  kuisaidia timu yake kupata pointi sita katika michezo miwili iliyocheza.

Singida iliifunga Kagera Sugar bao 1-0, pia ikapata ushindi kama huo dhidi ya Azam FC, michezo ambayo Gomez alionesha kiwango kikubwa, ambapo Gomez aliwashinda Ibrahim Abdallah wa Namungo na Henock Mayala wa Polisi Tanzania alioingia nao fainali.

Kwa upande wa Pluijm aliwashinda Roberto Oliveira wa Simba na Nasredeen Nabi wa Yanga alioingia nao fainali, baada ya kuiongoza Singida Big Star kushinda michezo miwili iliyocheza mwezi huo na kuendelea kushika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi.

Pia Kamati ya Tuzo imemchagua Meneja wa Uwanja wa  Highland Estates Mbarali, Omari Malule kuwa Meneja Bora wa Uwanja kwa mwezi Januari, kutokana na kufanya vizuri katika menejimenti ya matukio ya michezo pamoja na masuala yanayohusu miundombinu uwanjani.

 

 

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button