Wachinja Ng’ombe sita ufunguzi wa Zahanati

SONGWE: Wananchi wa Kijiji Cha Senga Kata ya Kamsamba wilayani Momba Mkoani Songwe wamechinja ng’ombe sita kusherekea kufunguliwa Zahanati inayotegemewa kupunguza vifo vya mama na watoto wachanga  hasa wakati wa kujifungua vilivyokuwa vikitokea katika Kijiji hicho.

Wakiongea na HabariLeo katika ufunguzi wa Zahanati Hiyo inayotegemewa kuhudumia zaidi ya Wananchi 5000 wa kijiji hicho na Vijiji jirani wamesema changamoto za akina mama kujifungulia njiani  na wengine kufia njiani zitapungua.

Mwenyekiti wa Kijiji Senga Cloud Mpepo amesema walianza kujenga Zahanati Hiyo mwaka 2010 baada ya kuona changamoto za wanawake wengi kujifungulia njiani wakati wanasafiri kufuata huduma kituo Cha afya kamsamba kilichopo umbali wa zaidi ya km 12.

Naye Verena Mbanga mkazi wa Kijiji Cha Senga amesema kutokana na umbali wa kufuata huduma za afya akina mama wengi walikuwa wanajifungulia nyumbani kwa kuhofia gharama za usafiri ambapo kwa pikipiki hutumia Sh.30000 kwenda na kurudi.

Akizundua zahanati Hiyo Mbunge wa Jimbo la Momba Condester Sichalwe amesema Zahanati Hiyo imechukua miaka 10 mpaka kukamilika kwake, ambapo amewapongeza Wananchi wa Senga kujitoa na kwa kiasi kikubwa kukamilisha Zahanati hiyo.

 

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button