Mkandarasi Kariakoo atakiwa kuharakisha

DAR ES SALAAM: MKANDARASI anayekarabati soko la Kariakoo Estim Construction Limited
ametakiwa kuongeza kasi ya kukamilisha mradi huo ili taratibu za kuwarejesha
wafanyabiashara zikamilishwe.

Kauli hiyo imetolewa leo Oktoba 31, 2023 na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Miundombinu , Mhandisi Rogatius Mativila mara baada ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa mradi huo uliofikia asilimia 91.

“ Mradi wa ukarabati na ujenzi wa soko la Kariakoo hadi sasa umefikia asilimia 91 na utakamilika hivi karibuni ambapo tunategemea zaidi ya wafanyabiashara 3,500 wapate nafasi za kufanya biashara katika mazingira ya kisasa.

Amesema, serikali inataka kuona mkandarasi akiongeza kasi katika ukarabati wa soko hilo unaogharimu Sh bilioni 28.3 ili shughuli za kiuchumi ziweze kuendelea sokoni hapo.

Kwa upande wake Kaimu Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo Sigsibert Valentine amesema maandalizi ya taratibu za kuwerejesha wafanyabiashara sokoni yanaendelea na utakuwa ni wa uwazi.

Mradi huo unatekelezwa kufuatia janga la moto lililotolea Julai 10, 2021 ambapo serikali imetoa Sh bilioni 28.

03 kufanikisha ujenzi na ukarabati ulioanza Januari 2022 na ulitarajiwa kukamilika Oktoba mwaka huu,

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button