Tanzania, taasisi Malysia kushirikiana sekta ya uvuvi

TANZANIA na Taasisi ya WorldFish kutoka Malaysia wamekubaliana kushirikiana kuimarisha sekta ya uvuvi ili kuwa na mchango mkubwa nchini sambamba na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Hatua hiyo imekuja baada ya leo Disemba 4, 2023 Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu, Essam Yassin Mohammed wa Taasisi ya Utafiti na Ubunifu katika minyororo ya thamani ya  uvuvi na ukuzaji viumbe (Worldfish) katika Mkutano wa COP 28, Dubai, UAE.

Aidha, pamoja mambo mengine, wamekubaliana kuhakikisha taasisi hiyo inaweka nguvu katika afua za kupambana na athari za  mabadiliko ya tabianchi ikiwemo uoteshaji wa matumbawe, kupunguza upotevu wa mazao ya uvuvi  baada ya kuvunwa,  kukuza ukuzaji viumbe maji bahari na kuboresha kosaafu za viumbe maji wakuzwao huku akimkaribisha kufungua ofisi ya WordFish nchini Tanzania.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button