“Wapeni fursa sawa watoto wenye ulemavu wa akili”

DAR ES SALAAM; Jamii imetakiwa kuhakikisha watoto wenye ulemavu wa akili wanapata fursa sawa za elimu na maendeleo katika jamii husika.
Wito huo umetolewa leo Machi 21, 2024, katika maadhimisho ya Siku ya watoto wenye ulemavu wa akili duniani katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha uelewa sahihi na kuondoa dhana potofu kuhusu watu wenye ulemavu wa akili.
Ofisa Elimu wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Hussein Mghewa akimwakilisha Mkuu wa wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo ameeleza umuhimu wa kujenga jamii yenye uelewa na unyenyekevu kwa wenye ulemavu wa akili.
Shughuli mbalimbali zimefanyika katika maadhimisho hayo ikiwa ni pamoja na maonesho ya vipaji vya watoto hao.



