Rutunga apewa kifungo miaka 20 jela

RWANDA : MAHAKAMA nchini Rwanda imemkuta na hatia Venant Rutunga  kwa kushiriki mauaji ya kimbari ya mwaka 1994, na kumuhukumu kifungo cha miaka 20 jela.

Venant Rutunga mwenye umri wa miaka 75, alirudishwa nchini Rwanda kutokea Uholanzi mwaka 2021 ili aweze kufunguliwa kuhusiana na mauaji hayo.

Hatahivyo upande wa mashtaka umethibitisha Rutunga kuhusika na mauaji  ya Kimbari kutokana na kuthibitika alikuwepo katika eneo hilo wakati mauaji hayo yalipofanyika.

SOMA : Ufaransa yasafishwa tuhuma mauaji ya kimbari Rwanda

Hatahivyo Rutunga  amekana mashtaka huku akidai aliwaita maafisa hao ili kulinda usalama, uamuzi ambao alisema uliidhinishwa na bodi ya wakurugenzi ya ISAR.

Habari Zifananazo

Back to top button