Ulaya wakubali Gonzalez ndiye Rais

ULAYA : BUNGE la Ulaya limepitisha azimio la kumtambua mgombea wa upinzani wa Venezuela Edmundo Gonzalez Urrutia kuwa rais halali wa nchi hiyo

Bunge hilo limesema pia kuwa viongozi wa Ulaya wanatakiwa kufanya kila liwezekanalo ili kumuwezesha kuchukua madaraka ifikapo Januari 10 mwakani.

Kura zilizopigwa na kupitishwa kwa kura 309 dhidi ya 201 ambao wengi  waliafiki makubaliano hayo.

Hata hivyo, maamuzi ya kura hiyo si ya lazima kutekelezwa na serikali za mataifa wanachama na hayawezi kubadilisha msimamo wa nchi za Umoja wa Ulaya.

SOMA :  Gonzalez aahidi mapambano

Gonzalez Urrutia mwenye umri wa miaka 75, ambaye alikimbilia nchini Uhispania, anadai kuwa ndiye mshindi wa uchaguzi wa urais wa Julai huku rais aliye madarakani, Nicolas Maduro, akidai pia kuwa alishinda muhula wa tatu wa miaka sita katika uchaguzi uliogubikwa na utata.

 

Habari Zifananazo

Back to top button