VENEZUELA : KIONGOZI wa upinzani nchini Venezuela Edmundo Gonzalez, ameahidi kuendeleza mapambano dhidi ya Rais wa Venezuela Nicolas Maduro hata kama yuko nje ya nchi.
Gonzalez ambaye kwa sasa amekimbilia nchini Hispania amesema ataendelea kupigania demokrasia ili kuhakikisha Venezuela inaharakisha maendeleo yake.
Kiongozi huyu wa upinzani aliamua kukimbilia Hispania baada ya mahakama ya Venezuela kutoa waranti wa kumkamata.
Gonzalez aliwasili nchini Hispania hapo jana na serikali nchini humo imeshampatia hifadhi .
Marekani na nchi kadhaa za Amerika Kusini, zinaamini Edmundo Gonzalez alishinda uchaguzi wa urais uliofanyika Julai nchini Venezuela .
SOMA : Polisi wadhibiti maandamano Venezuela
Hatahivyo Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken, amesema hatua ya Gonzalez kuikimbia nchi yake ni kielelezo tosha cha sera zinazoenda kinyume na demokrasia nchini Venezuela.