Polisi wadhibiti maandamano Venezuela

VENEZUELA: Vikosi vya usalama nchini Venezuela vimerusha mabomu ya kutoa machozi na risasi za mpira dhidi ya raia walioamua kuandamaana dhidi ya matokeo ya uchaguzi.

Maelfu ya watu walikusanyika katika maeneo mbalimbali mjini Caracas huku wengine wakitembea umbali  mrefu kutaka kuelekea Ikulu ya rais.

Kambi ya upinzani nchini humo imeendelea kupinga ushindi wa Rais Maduro na kuuchukulia kama ulaghai, huku wakisema mgombea wao Edmundo González alishinda kwa kishindo kwa kupata asilimia 73.2 ya kura.

Advertisement

Awali vyama vya upinzani viliungana ili kutaka kumng’oa Rais Maduro baada ya kukaa madarakani kwa miaka 11, huku kukiwa na hali ya kutoridhika iliyoenea kutokana na kudorora kwa uchumi nchini humo.

Nchi kadhaa za Magharibi na Amerika Kusini, na mashirika ya kimataifa ikiwemo UN, wametoa wito kwa mamlaka ya Venezuela kutoa taarifa za upigaji kura kwa lengo la kuwasaidai wananchi nchini humo kufahamu nani ameshinda uchaguzi huo.

SOMA:  Polisi Kenya wapiga marufuku maandamano Nairobi

Kundi kubwa la wanajeshi na polisi, ikiwemo mabomu ya kutoa machozi, walionekana kwenye mitaa ya Caracas waliamua kuwatawanya waandamanaji na kuwazuia kukaribia ikulu ya rais.

/* */