Man United yaandaa dau kumsajili Kolo Muani

TETESI za usajili zinasema Manchester United imeandaa ofa ya pauni milioni 58.6 kumsajili fowadi wa Paris Saint-Germain, Randal Kolo Muani, 25.(Fichajes, via Teamtalk)

Galatasaray inataka kufanya uhamisho wa mkopo wa mshambuliaji wa Nigeria, Victor Osimhen kutoka Napoli kuwa dili la kudumu huku Chelsea bado ikionesha kuwa na nia kumsajili.

Hata hivyo, Osimhen mwenye umri wa miaka 25 atagharimu pauni milioni 68 Januari au pauni milioni 63 majira yajayo ya kiangazi.(Corriere dello Sport – in Italian)

SOMA: Tetesi za usajili Ulaya

Manchester City inafikiria kumsajili golikipa wa Porto, Diogo Costa, 25, kama mbadala wa Ederson, lakini mlinda lango huyo wa Ureno atagharimu pauni milioni 63. (Caught Offside)

Manchester United imemweka beki wa kulia wa Chelsea, Ben Chilwell, 27, kuwa lengo kuu usajili Januari, 2025. (Teamtalk)

Kiungo wa Hispania, Martin Zubimendi amesisitiza msimamo wake kubaki Real Sociedad licha ya nia ya kumsajili kutoka Manchester City.(Mirror)

Crystal Palace itaimarisha kumfuatilia fowadi raia wa Ivory Coast anayekiwasha klabu ya Hammarby ya Sweden, Bazoumana Toure, 18, ambaye pia anawindwa na timu za Manchester United na Celtic.(Give Me Sport)

Arsenal bado itahitaji kusajili mshambuliaji wakati wa dirisha dogo la usajili Januari, 2025 licha ya fowadi wa kijerumani Kai Havertz, 25 kuanza vizuri msimu. (Football Insider)

Habari Zifananazo

Back to top button