Simone Inzaghi akubali kumrithi Ten Hag

TETESI za usajili barani Ulaya zinasema tayari kocha wa Inter, Simone Inzaghi amekubali kumrithi Erik ten Hag kama Β kocha wa Manchester United kwa ajili ya msimu wa 2025/26. (InterLive – Italy)

Kocha wa Manchester United, Erik ten Hag.

Wakati huo huo mshambuliaji wa Man Utd, Joshua Zirkzee amepata dili kurejea Serie A kukiwasha Juventus wakati wa dirisha la uhamisho Januari, 2025. (JuveLive – Italy)

Manchester City na Newcastle United zote mbili zimeonesha nia kumsajili fowadi wa Barcelona, Raphinha, ambaye ana thamani ya pauni milioni 83.1. (Fichajes – Spain)

SOMA: Ten Hag: Rashford hauzwi

Tottenham Hotspur itahitaji kulipwa pauni milioni 80 ili kuachana na beki wake wa kulia Pedro Porro, ambaye anawindwa na Man City na Real Madrid. (Football Insider)

Pia kiungo wa Tottenham, Archie Gray, 18, anahusishwa kuondoka klabu hiyo huku Sevilla ikifukuzia dili la mkopo. (Mucho Deporte – Spain)

Borussia Dortmund inataka kusajili beki mpya wa kushoto Januari, 2025 na imeelezea nia yake kuhitaji huduma za Ben Chilwell wa Chelsea na Milos Kerkez anayekiwasha Bournemouth. (TEAMtalk)

Habari Zifananazo

Back to top button