ICC yaombwa kuchunguza mauaji ya waandishi

UFARANSA : SHIRIKA la kimataifa la Waandishi Habari wasiokuwa na Mipaka, RSF limesema waandishi wa habari 54 wameuawa duniani ambao wengi wameuawa wakiwa kazini 2024.
Kwa mujibu wa ripoti ya kila mwaka ya shirika hilo limeeleza kuwa theluthi moja ya waandishi wa habari wameuawa katika Ukanda wa Gaza.
Hadi sasa idadi ya waandishi habari waliouawa kulingana na takwimu za mwezi Novemba ziko sawa na kiwango cha mwaka uliopita. SOMA: Gaza yaongoza vifo vya wanahabari
Unaambiwa waandishi 31 kati ya 54 waliuawa katika maeneo ya mizozo ya vita na kufanya idadi hiyo kuonekana kubwa katika kipindi cha miaka mitano.
Hatahivyo, RSF imeitaka Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ya ICC kuanza kuchunguza mauaji ya wafanyakazi wa vyombo vya habari kama uhalifu wa kivita.