BRUSSELS : WAANDISHI wa habari wapatao 104 wameuawa duniani mwaka 2024.
Taarifa hiyo imetolewa mjini Brussels nchini Ubelgiji kwa vyombo vya habari na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Kimataifa la Wanahabari –IFJ, Anthony Bellanger amesema mwaka huu kumekuwa ongezeko kubwa la vifo vya wanahabari ukilinganisha na miaka iliyopita.
Bellanger amesema vifo vingi vya wanahabari vimetokana kufuatia mizozo mbalimbali ya vita inayoendelea kutokea katika mataifa mbalimbali kama huko Palestina ambapo waandishi wengi wameripotiwa kupoteza maisha..
Bellanger amesema kuna wanahabari wengine ambao wamekamatwa 520 ambao mpaka leo wako gerezani bila sababu za msingi. SOMA: Watoto 260 wauawa vurugu Palestina
Maeneo yaliyotajwa kuongoza kwa vifo vya wanahabari ni Mashariki ya Kati, Asia-Pasifiki na Ulaya hasa kutokana na vita vinavyoendelea nchini Ukraine.