Benjamin Mkapa yapandikiza figo mgonjwa wa 50, yaokoa bil 1.6/-

HOSPITALI ya Benjamin Mkapa (BMH) ya mkoani Dodoma imefanikiwa kumpandikiza figo kwa mafanikio mgonjwa wa 50 tangu kuanza kutoa huduma hiyo miaka sita sasa huku Sh bilioni 1.6 zikiokolewa.

Emmanuel Woiso (38) ambaye ni mgonjwa wa 50, jana alipandikizwa figo na hospitali hiyo iliyoanza kutoa huduma ya bingwa bobezi ya kupandikiza figo Machi 22, 2018.

Mgonjwa huyo ameruhusiwa kurudi nyumbani na kuendelea na shughuli zake. Akizungumza wakati wa kumruhusu Woiso kutoka hospitalini jana, Mkuru genzi Mtendaji wa BMH, Profesa Abel Makubi alisema mgonjwa huyo kuruhusiwa ni mafanikio makubwa katika huduma za kibingwa bobezi zinazotolewa na wataalamu wazawa.

Alimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuen deleza kufanya uwekezaji mkubwa katika sekta ya afya hususani katika huduma za ubingwa bobezi ambazo awali zilikuwa zikipatikana nje ya nchi tu.

“Takribani miaka sita ili yopita Hospitali ya Benjamin Mkapa ilikuwa kituo cha pili hapa nchini kutoa huduma ya bobezi ya upandikizaji figo hiyo ambapo kati ya wagon za matibabu hayo, Profesa Makubi alisema kwa sasa gharama ya matibabu kwa mgonjwa mmoja ni wastani wa Sh milioni 34 ikilinganishwa na wastani wa Sh milioni 64 kama mgonjwa huyo angetibiwa nje ya nchi India na Ulaya.

Wagonjwa hao 50 waliopandikizwa hapa Benjamin Mkapa, asilimia 95 wanaishi na kuendelea na majukumu yao,” alisema Profesa Makubi.

Alisema takribani asilimia 98 ya wagonjwa wanaopan dikizwa figo wanaendelea kuishi na kufanya majukumu yao baada ya kipindi cha mwaka mmoja tangu kupata huduma hiyo, huku wastani wa asilimia 86 wakiendelea kuwa hai baada ya miaka mitano tangu kupata huduma.

“Hii inaonesha ubora wa huduma hii hapa nchini kuwa ni mzuri kwa viwango vinavyofanana na maeneo mengine duniani kama Marekani, Ulaya na India,” alieleza.

Akizungumzia gharama “Hivyo kupandikiza figo wagonjwa hao 50 tangu Hospitali ya Benjamin Mkapa kuanza kutoa huduma ya ub ingwa bobezi wa upandikiz aji figo, serikali imetumia takribani Shilingi bilioni 1.7 ikilinganishwa na takribani Shilingi bilioni 3.3 endapo wananchi hao wangetibiwa nje ya nchi, hivyo kuokoa takribani Shilingi bilioni 1.6,” alifafanua Profesa Makubi.

Alisema mwelekeo wa BMH katika mwaka 2025 ni kuongeza zaidi kasi ya huduma za upandikizaji figo kwa kutumia teknolojia za kisasa zaidi za upasuaji na uvunaji figo kwa njia ya matundu madogo badala ya kupasua sehemu kubwa ya mwili katika kuvuna figo.

Pia, itajikita katika ku wekeza katika upasuaji wa kutumia roboti ambazo hura hisisha kazi kwa watalaamu.

“Tuna kituo chetu cha matibabu ya figo tunakwenda kukipanua kiwe kituo cha umahiri cha upandikizaji wa figo hapa nchini na Afrika” alieleza

Habari Zifananazo

Back to top button