Samaki waanza kushuka, nyama bado juu Dar

DAR ES SALAAM: BEI za vitoweo katika Mkoa wa Dar es Salaam zimeendelea kuimarika huku nyama ikiendelea kuwa juu ikiuzwa kwa Sh 11,000 hadi 13,000 kwa kilo.
Akizungumza na HabariLEO jana Ofisa Mifugo na Msimamazi wa Kanda ya Kati Bodi ya Nyama Tanzania, John Chiboma alisema kupanda kwa bei ya nyama kabla na baada ya Sikukuu ya Krisimasi na Mwaka Mpya kumesababishwa na malisho hafifu ya mifugo yaliyosababishwaa ukosefu wa mvua.
Alisema hali hiyo imesababisha mifugo mingi kukosa ubora ambao unakidhi haja ya wanunuzi sanjari matak wa ya soko la nyama.
“Tumetoka ka tika msimu wa kiangazi mifugo mingi inakosa ubora unaokidhi kuingia sokoni kutokana malisho kutokuwa na nyasi za ku tosha, hivyo mifungo inayoingia sokoni inakuwa ni michache wakati uhitaji mkubwa ndio maana bei inapanda,” alisema.
Chiboma alitaja sababu nyingine ya bei ya nyama kupanda ni kuwa baadhi ya wafugaji wanashiriki katika shughuli nyingine za kiuchumi ikiwemo kilimo, hivyo wengi wao wanajikita katika uandaaji wa mashamba na kuweka pembeni shughuli za mifugo.
“Bei bado ipo juu, wiki iliyopita tulikuwa Morogoro kilo moja inauzwa 10,000 hadi 11,000 na Dodoma pia wakati kipindi cha nyuma ilikuwa ikiuzwa shilingi 8,000 hadi 9,000 ila tunategemea kuanzia Februari bei itashuka kwa sababu mvua zimeanza kunyesha na pia shughuli za mashambani zitakuwa zimepungua,” alisema.
Mteknolojia wa Samaki na Ofisa Uvuvi Soko la Samaki Feri, Amina Hamidu alisema kuwa bei ya samaki katika soko hilo imeshuka kwa mwezi huu ikifananishwa na Desemba mwaka jana.
Alisema kuwa Desemba bei ya samaki ilipanda kutokana na hali ya upepo uliosababisha kuadimika kwa samaki sokoni hapo. “
Bei ilipanda kwa mfano dagaa mchele ndoo ilifika hadi 150,000 wakati kipindi kingine bei ya juu inakuwa 100,000 na wanauzwa hadi 75,000, 60,000 inategemea na ubora wake,” alisema.
Amina alisema samaki wengine wameendelea kununuliwa kwa bei ya kawaida na kuuzwa kwa bei ya kawaida isipokuwa samaki aina ya ngisi.
Alisema ngisi wamepanda bei kwa sababu hawavuliwi kwa wingi kwa sababu si msimu wake hali inayosababisha kuongezeka kwa uhitaji. “Samaki wengine bei ipo kawaida kwa mfano vibua wanauzwa 230,000 hadi 200,000 kwa ndoo lakini ngisi wapo juu mfano leo (jana) asubuhi mnadani wameuza kilo kwa 25,000 na sasa hivi kilo imesimama 18,000,” alisema.
“Ngisi wanapatikana kwa wingi wakati wa mbalawezi kali, lakini kwa sasa mbalamwezi bado haijawa kali ila hadi kufikia mwezi ujao watakuwa wamechangan ya katika upatikanaji wake na bei itakuwa chini kama zamani ambapo wa saizi ya kati wanauzwa hadi 12,000 na wakubwa 15,000 kwa kilo,” aliongeza.
Kwa upande wake, mfanyabiashara wa kuku soko la Shekilango, Manoma Hassan alisema kuwa kwa sasa kuku wanauzwa Sh 6,800 hadi 7,000 kutokana na wingi wa kuku kutoka kwa wafugaji sokoni hapo.
Manoma alisema De semba mwaka jana kuku aliuzwa kati ya 7,200 hadi 12,000 kulingana na uzito wa kuku.
“Mwezi uliopita kuku wa kilo moja na nusu aliuzwa hadi 12,000, mwe nye kilo moja aliuzwa 8,000 hadi 9,000 lakini kuanzia Januari 10 bei zitashuka itarudi kama kawaida 7,000 hadi 6,800,” alisema.
Alisema kuwa bei ya kuku inategemea na wingi wa kuku wanaofikishwa sokoni hapo, “Kuna siku kuku wanakuwa wengi ndio bei inashuka, la kini kuna siku wanakuwa adimu hivyo mtu akija nao anapanga bei yake ambayo yeye anaona inamfaa”