Rais Mwinyi awakaribisha wawekezaji kutoka Uingereza

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Ali Mwinyi amewakaribisha wawekezaji kutoka Uingereza kuwekeza  Zanzibar katika fursa mbalimbali ikiwemo sekta ya uchumi wa buluu, utalii, usafiri wa baharini, uvuvi, nishati na miundombinu ya kidijitali.

Dk Mwinyi amesema hayo alipojumuika kwenye chakula cha jioni na wakurugenzi wa taasisi mbalimbali za biashara na uchumi za Uingereza kilichoandaliwa na Taasisi ya Eastern Africa Association ya Uingereza katika Jiji la London Aprili 7, 2025.

Aidha, Rais Dk Mwinyi amesema katika kipindi cha  miaka minne uchumi wa Zanzibar unaendelea kukua zaidi  ya asilimia 7 kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanyika katika sekta mbalimbali.

Dk Mwinyi ametoa wito kwa  wawekezaji hao  kuwekeza katika zao la mwani, ameeleza kuwa Zanzibar ndio  mzalishaji namba moja wa zao hilo Afrika ambalo soko lake linaendelea kukua zaidi.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button