XI Jinping yuko Cambodia

CAMBODIA : RAIS Xi Jinping wa China amewasili Cambodia ambapo kitakuwa kituo cha mwisho cha ziara yake ya kuyatembelea mataifa matatu ya kusini mashariki mwa Asia.

Akizungumza na vyombo vya habari nchini humo,  Xi ameiomba nchi hiyo kushirikiana na China kupambana dhidi ya mfumo unaotegemea nguvu za taifa moja duniani, siasa za mabavu na mivutano isiyo na tija.

Amesema nchi hizo mbili ni lazima zikatae sera za kufunga milango na badala yake zipigie debe kuendeleza ushirikiano katika ngazi ya kimataifa.

Cambodia iliyo msafirishaji mkubwa wa nguo kwenda Marekani, iliwekewa ushuru wa asilimia 49 na utawala wa Donald Trump ambao umesitishwa kwa muda hadi mwezi Julai.

Viongozi wa nchi hiyo wanatumai ziara ya Xi itasaidia kupatikana msaada zaidi wa kifedha ikiwemo miundombinu. SOMA: China yaapa kulinda maslahi ya kitaifa

 

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button