CHINA: SERIKALI ya China imeapa kulinda maslahi yake ya kitaifa baada ya rais wa Marekani Donald Trump kusema kwamba ushuru wa forodha wa asilimia 10 kwa bidhaa za China unaweza kuanza kutekelezwa kuanzia Februari mosi.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Mao Ning, alifafanua msimamo huo akisema kwamba taifa hilo linaamini hakuna mshindi katika vita vya kibiashara au ushuru, hivyo litaendelea kulinda maslahi yake.
Trump alieleza kuwa kuna haja ya kurekebisha uwiano wa kibiashara kati ya Umoja wa Ulaya na Marekani, akidai umoja huo haununui bidhaa za kutosha za Marekani, na hivyo angetafuta suluhisho kwa kuongeza ushuru au kuishawishi Ulaya kununua zaidi mafuta na gesi kutoka Marekani.
SOMA: Asali kukuza uchumi wa Tanzania, China