Uturuki kulijengea uwezo jeshi la zimamoto Tanzania

DAR ES SALAAM: UTURUKI imesema itaendelea kushirikiana na Tanzania kulijengea uwezo Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ili kukabiliana na majanga, dharura pamoja na ajali mbalimbali.

Aidha, taifa hilo linatarajiwa kuwachukua askari 10 wa jeshi hilo kutoka Tanzania kwa ajili ya kuwapeleka mafunzoni nchini Uturuki.

Wakizunguza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kuhitimisha zoezi la mafunzo ya utayari kwa askari 35 wa kitanzania kupitia Shirika la Uratibu na Maendeleo la Uturuki (TIKA).

Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Bakir Gezel Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la TIKA, Feliz Sahic pamoja na Mkurugenzi wa Manispaa ya Konya Ibrahim Navruzi wamesema kutokana na mahusiano mazuri baina ya mataifa hayo mawili nchi ya Uturuki imeridhia awamu nyengine ya mafunzo kwa askari 10 yakafanyike nchini uturuki ili kuendekeza mafunzo yaliyofanyika nchini ambayo wamesema yamefanikiwa kwa zaidi ya asilimia 95.

Kamishina Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini Tanzani,a John Mwasunga amesema ili kujenga jeshi imara la zimamoto na uokoaji litakaloendana na mafunzo hayo ya kisasa Rais Samia ameridhia Sh bilioni 260 kununua vifaa vya kisasa kwa ajili ya shughuli za uokoaji na kuzima moto.

Amesema tayari vifaa hivyo vimeshanunuliwa ikiwemo magari ya kuzimamoto zaidi ya 150, magari ya kubeba wagonjwa,magari ya oparesheni pa moja na helikopta moja kwa ajili ya kufanya kazi ya maokozi na uzimaji moto .

Naye  baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo Mkaguzi Msaidizi Singo Nyani kutoka Kituo cha Zimamoto Temeke wakizungumza wameshukuru kwa kupatiwa ujuzi na maarifa mapya hasa katika eneo la kutumia teknolojia ili kuokoa watu katika majengo marefu pamoja na namna ya kuzimamoto sanjari na kukoa majeruhi katika ajali za barabarani.

Katika mafunzo hayo yaliyodumu kwa siku kumi askari wa kutoka manispaa ya Konya nchini Uturuki wamewajengea uwezo askari 35 wa kitanzania katika maeneobalimbali ikowemo.kuzima moto,ajali mbalimbali,sanjari na namna ya kuokoa watu katika majengo yaliyoporomoka kama vile maghorofa ambapo mafunzo  hayo yalikuwa kakitoa nadharia na vitendo

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button