Rais Samia: Simba mmeipa heshima kubwa nchi yetu

DURBAN; RAIS wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hasan, ameipongeza klabu ya Simba kwa kufuzu fainali a michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika na kuahidi kuwa wana hamasa yake wakati wote.
Rais Samia ameandika kwenye ukurasa wakewa mtandao wa kijamii: :Pongezi za dhati kwa Klabu ya Simba kwa ushindi katika mchezo wa Mashindano ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF Confederation Cup), na kuandika historia ya kufika fainali ya mashindano haya. Mmeipa nchi yetu heshima kubwa. Nawatakia kila kheri. Mnayo hamasa yangu wakati wote.”

Simba imetinga fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, baada ya leo kutoka 0-0 mchezo wa marudiano nusu fainali dhidi ya wenyeji wao Stellenbosch FC ya Afrika Kusini Uwanja wa Moses Mabhida mjini Durban.
Kutokana na matokeo hayo Simba imesonga mbele kwa jumla ya bao 1-0 kutokana na ushindi iliyoupata mchezo wa kwanza baina ya timu hizo uliofanyika Jumapili iliyopita Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar.



